Nina miaka zaidi ya 30 sina ninachomiliki, nahisi kukata tamaa. Msaada wenu

Sema una miliki na digrii,vipi mzee wako alikupokea? Au bado anakuona kibaka tu.
 
Sina kazi, sina kibarua kabisa. Maisha yamekuwa magumu sana upande wangu.


Shida ipo hapo, bila ya kazi utamiliki nini??!!----- tafuta kazi kwanza ndipo utapata malipo na hatimaye utaanza kumiliki vitu mbalimbali.

Kuhusu kazi, zipo kazi nyingi za halali unazoweza kufanya kwani katika umri wako bado nafasi unayo ya kujishughulisha na kuwa na mali.

Kuna; kilimo, Biashara, uvuvi, ufundi, ujenzi, uchimbaji madini (kokoto, rubi, dhahabu nk), umachinga, hizi ni kazi zisizohitaji taaluma yeyote, baada ya hapo unaweza kutafuta nafasi yoyote ya ajira nk, jambo jingine using'ang'anie kuishi mahali pamoja, tembea ili upate EXPOSURE na kuona opportunities zaidi kwani kutembea ni kujifunza na kuvumbua mbinu mpya za maisha.
 

Unamiliki afya, hakuna kikubwa zaidi ya hicho, tumia afya yako kumshukuru Mungu na kumuomba akujaalie subira na akukadirie rizki itakayokufaa.
 
Kazi huzipati hapa! Change your mind set you will get into the game!
 
Pole sana mkuu. Usikate tamaa, pambana. Mimi hali ilibadilika nilipofikisha miaka 35 baada ya kusota kama wewe!
Ushauri: Usichague kazi, fanya kazi yoyote inayokuja mbele yako na umtegemee Mungu.
 
Sijaona chaa ajabu hapo. Kiuchumi kweli upo nyuma kwa umri huo.... Ila kiuhalisia haujafeli maisha bado mapema sana kukata tamaa...... Ungekuwa na ungojwa usio na tiba ningesema ni kweli. Ila wewe bado kijana sana kwa mwanaume kukata tamaa.

Imagine kuna wanawake wapo umri kama wako, hawajaolewa hawana kazi na hawana mtoto...... Imagine wanajisikiaje sasa kwa wewe mwanaume still una nafasi ya kupambana na kuweka mambo sawa.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtu wangu wa karibu ambaye ninamfahamu, ambaye pia alikuwa na hisia kama zako. Ilifikia kiwango mpaka wazazi wake walianza kumnanga wazi wazi tena mbele ya wadogo zake. Aliamua kwenda Mbuguni Arusha kwenye machimbo ya vito vya thamani. Alisota na hatimaye akaibuka, kwa sasa ana ukwasi wa haja.

Ebu na wewe jaribu kulishughulisha na mambo ya kilimo, ukijizatiti vyema hakitakuangusha. Ama kama unapenda kazi za mitulinga tafuta "connection" ktk mgodi mmojawapo uende kujaribu bahati yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesahau, una na smartphone mkuu!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama unamiliki ‘dushelele’ na lipo murua kabisa inatosha kwa umri wako, andaa plan yako ya maisha kwa miaka 10 ijayo, igawe kwenye long & short term plan......,,
 
Mbona wapo wakubwa zaidi yako hawana hata godoro?
Jivunie ulipo leo huku ukiongeza juhudi na kujiahirikisha na wale wanaofanikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…