Nina miaka zaidi ya 30 sina ninachomiliki, nahisi kukata tamaa. Msaada wenu

Nina miaka zaidi ya 30 sina ninachomiliki, nahisi kukata tamaa. Msaada wenu

Kitabu cha Mhubiri kinasema kila jambo lina wakati wake, lakini pia Mungu akitaka kukupa kitu huwa haandiki barua.Jipe moyo, tafuta vibarua na mtumaini Mungu.Wengine hufanikiwa mapema ila huchelewa kufanikiwa. Pia kumbuka Mwenyezi Mungu yupo na wale wenye subira.
Naombeni msaada wenu wakuu ambao waliokwisha pitia hali kama hii ninayopitia mimi. Nina miaka 30 na kitu, sina ninachomiliki zaidi ya godoro langu, radio ndogo ya muziki, vyombo vya udongo ndani ya beseni pamoja na nguo zangu.

Nahisi kukata tamaa kabisa na haya maisha. Mliokwisha pitia hali kama hii yangu kwenye umri huu na ukawa kwenye maisha kama haya, ilikuwaje? Naombeni mnisaidie kimawazo.

Kuna muda natamani hata corona ije upande wangu, nahisi kukata tamaa kabisa.

Sina kazi, sina kibarua kabisa. Maisha yamekuwa magumu sana upande wangu.

Karibuni kwa mawazo yenu, wakuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa yangu yeye alipoachwa na mwanamke wake alipoteana sana, maana aliwekeza zaidi kwenye mapenzi kuliko maisha
Kiukweli aliona sasa dunia imefika ukomo

Siku aliyoamka akasema nitasimama tena, akaweka shida chini akainua mikono juu

Saa hii ana familia yake, ana nyumba na mambo yanaenda

Kuna nyakati unaweza kuona sasa huwezi kuendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha yetu vijana wa kileo yanakatisha tamaa sana endapo utakuwa unaangalia vijana wenzetu waliofanikiwa katika umri mdogo. Ni zao la kujituma na bidii hasa wale ambao hawakupoteza muda mwingi madarasani.

Cha muhimu ni kukimbizana na muda na kujiwekea milestones. Kwa kawaida katika umri wa miaka 30 ni umri ambao kijana unatakiwa uwe na stable income kwa namna yeyote but most likely kuajiriwa au kutoa huduma flani kisha ulipwe. Inaaminika ni umri pekee ambao utakuwa umemaliza pilikapilika za kusoma. Hapo ndio maisha yanaanza sasa maana ukishakuwa na stable income ni rahisi kujiwekea mipango na kuitekeleza mmoja baada ya mwengine.

Shida tuliyonayo vijana wa sikuhizi ni kukosa ajira ikiwa mtu ulisoma kwa nguvu na muda mrefu ila mwishowe kazi kupata ni kipengele. Ukicheki hukuwahi kuwa na contigency plan endapo kupata mchongo kutabuma unachobakiwa nacho ni Ego tu kuwa mi ni msomi nikapige kiwi kweli? Mzazi wangu atanionaje? Wadogo zangu nao duh. Marafiki watanionaje? Hii hali ndio inatulostisha utashangaa umegonga 30 huna muelekeo.

All in all ni kukaza tu, ushauri wangu ni focus tu. Focal point iwe ni kutengeneza pesa at any cost,ukitaka kumuua nyani usimuangalie usoni mkuu. Futa kitu kinaitwa aibu maana pesa haimfuati mtu anayeona aibu kuitafuta katika mazingira yeyote.

Piga plan ya miezi 6 tu ingia biasharani na fanya biashara ambazo ni service based rather than product based. Namaanisa tafuta ujuzi flani wa kawaida tu unaeza hata mpanga mtu akakufundisha kupaka rangi kucha wanawake na kuwabandika ukaanza na hilo. Naamini course haitazidi week 1 kisha utatawanyika kitaa na bag lako lenye mazaga zaga kumbuka ukitafta pesa ni kama kumuua nyani usimuangalie usoni i.e aibu tupa pembeni kisha jiamini wewe ni mpambanaji. Baada ya miezi 6 utakuwa umesogea toka ulipo na kuchungulia fursa zaidi za kuboresha kipato kwa jinsi ambavyo unazunguka kitaa.
 
Madhara ya kuchagua kazi matokeo yake ndio kama hivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahah hii kitu inapoteza vijana wengi sana mkuu, katika maisha yangu sikuwahi kuwaza ipo siku ntakaanga kitimoto na kuwafungulia watu bia. Ila ilifikia stage nikaona i have to do something for my self-development.

Maisha yatatukaza always cha msingi ni kubadilisha style tu ya kupigwa mashine ili usiumie sana ila kukazwa kupo pale pale.🤣🤣🤣🤣🤣
 
Fanya tathmini juu ya mahusiano yako na jamii inayokuzunguka. Kwa muda mrefu unakuwa na watu wa aina gani. Kuna wengi wamefanikiwa kwa mtaji wa adabu, utii, nidhamu, bidii na uaminifu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa watu wapo sana, mie hupenda kuwaita chawa ama watu wa kujikomba komba. Al Haji Bashite ni mfano hai kabisa wa watu wa design hii.
Ukiweza kujikomba kwa wenye nazo pia ni kipaji ambacho kinaweza kukuvusha point A to B ndani ya muda mchache. Too bad sio wote ambao tumejaaliwa hiki kipaji.
 
Naombeni msaada wenu wakuu ambao waliokwisha pitia hali kama hii ninayopitia mimi. Nina miaka 30 na kitu, sina ninachomiliki zaidi ya godoro langu, radio ndogo ya muziki, vyombo vya udongo ndani ya beseni pamoja na nguo zangu.

Nahisi kukata tamaa kabisa na haya maisha. Mliokwisha pitia hali kama hii yangu kwenye umri huu na ukawa kwenye maisha kama haya, ilikuwaje? Naombeni mnisaidie kimawazo.

Kuna muda natamani hata corona ije upande wangu, nahisi kukata tamaa kabisa.

Sina kazi, sina kibarua kabisa. Maisha yamekuwa magumu sana upande wangu.

Karibuni kwa mawazo yenu, wakuu.
Muombe Bwana Mungu wako
 
Ni wakati wako wa kufikiria zaidi. Kosa kubwa Sana kukata tamaa. Hatua ya kimsingi ni lazima ujiulize Kwa Siku moja umefanya nini! Usione haya kufanya kazi yoyote na ili mambo yaende ondoka unapokaa nenda ugenini., Kama ni wa Mbeya nenda Mwanza
 
Usikate tamaa..
IMG_20200513_162300.jpg
 
Back
Top Bottom