Naombeni msaada wenu wakuu ambao waliokwisha pitia hali kama hii ninayopitia mimi. Nina miaka 30 na kitu, sina ninachomiliki zaidi ya godoro langu, radio ndogo ya muziki, vyombo vya udongo ndani ya beseni pamoja na nguo zangu.
Nahisi kukata tamaa kabisa na haya maisha. Mliokwisha pitia hali kama hii yangu kwenye umri huu na ukawa kwenye maisha kama haya, ilikuwaje? Naombeni mnisaidie kimawazo.
Kuna muda natamani hata corona ije upande wangu, nahisi kukata tamaa kabisa.
Sina kazi, sina kibarua kabisa. Maisha yamekuwa magumu sana upande wangu.
Karibuni kwa mawazo yenu, wakuu.
Kwanza, Habari ndugu. Usitake kufanya mambo makubwa mara moja. Kwa sasa inaonekana tatizo sio kwamba haujapata mali au wealth. Kuna watu wako hospitali hata kuandika hii post hawawezi.
Kwanza kabisa, jitahidi kushukuru Mungu kwa chochote ulicho nacho. Hata afya au simu na uwezo wa kuingia JF, ni jambo la kushukuru.
Pili, usijilinganishe na wengine.
Mara nyingi kijana kama wewe unaangalia watu wengine wa umri wako wa miaka 30 unaona kama wametoboa maisha. Kumbuka maisha ya watu wawili hayalingani. Wengine wamezaliwa katika utajiri, wengine walifanya madawa ya kulevya, wengine wameuza miili, na ndio wakatoboa.
Tatu, Ukishashukuru Mungu kwa mibaraka midogo, na ukishaacha kujilinganisha na wengine, basi sasa tafakari ni namna gani unaweza kupata fu
raha ndogo ndogo maishani kwa sasa. In English wanasema short term goals related to short term gratifications. Hapa angalia vitu kama chakula gani kikupe faraja nk. Basi jitahidi upate faraja hio ya sasa sababu uko very depressed.
Nne, ukishaweza hapo kwa short term goals, sasa angalia long term goals, au malengo ya kukuletea utajiri.
Kumbuka utajiri hauji mara moja tu paap. Success never happens overnight.
Utajiri ni matokea ya malengo mazuri, kuchapa kazi, kutokata tamaa, kujiamini, na kumwamini Mungu. Lakini hayo yatatokea baada ya kufanyia kazi lengo kwa muda mrefu. Kwa sasa long term goal
angalia upate ujuzi fulani mzuri wa kukupatia pesa nzuri. Au hata ujuzi wa kujiajiri. Jifunze vitu kama ufundi wa plumbing, welding, nk. N
a pambana upate ujuzi kwelikweli sio wa kubabaisha. Manake uwazidi wengine, ili hata uuze jina kwa matokea mazuri ya kazi zako.
Usihofu kuuliza kwa ushauri zaidi.