Nina Mil.10 Nikianza ujenzi wa nyumba itafika wapi??

Nina Mil.10 Nikianza ujenzi wa nyumba itafika wapi??

Rapunzel

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2012
Posts
1,079
Reaction score
599
Habari wa JF , naomba msaada wa kimawazo na ushauri, Nina Mil.10 ninaplan ya kujenga nyumba yenye vyumba 3,

Je kwa hiyo pesa nyumba yangu itaishia wapi?

Kwa wenye uzoefu wa mambo ya ujenzi tafadhari....
 
Inategemea na mahali ulipo,kwani gharama za ujenzi zinatofautiana sehemu hadi sehemu....uko wapi weye?
 
Habari wa JF , naomba msaada wa kimawazo na ushauri, Nina Mil.10 ninaplan ya kujenga nyumba yenye vyumba 3,

Je kwa hiyo pesa nyumba yangu itaishia wapi?

Kwa wenye uzoefu wa mambo ya ujenzi tafadhari....

eehe ngoja lara 1 akusikie!!
 
Kama walivyosema wengine ukijitahidi sana utafika lental, ila wewe anza kujenga na hongera kwa kupata mil 10 mingi eti.
 
Kwa utaratibu wa kawaida inakadiliwa nyumba ya kisasa inatumia laki 5 kwa kila square metre kwa nyumba yenye flôor moja.
 
Kama walivyosema wengine ukijitahidi sana utafika lental, ila wewe anza kujenga na hongera kwa kupata mil 10 mingi eti.

Asante mpendwa wangu, naomba mungu anisimamie..
 
eehe ngoja lara 1 akusikie!!

acheni kumpotosha mwenzenu ujasiliamali sio rahisi kihivyo, bearing risks in the risky Tanzanian business sio kazi ndogo. Btw hata nyumba nayo ni învestment tena ambayo ni secure and reliable.
 
Ndugu we anza tu mil 10 unajenga mpaka level ya lenta na kubakiwa na vijisent vyako
 
Nimefurahi sana mada hii kuiona, kwani mm nina m20, mchanga na mawe ya kutosha ninayo, eneo morogoro, room 3 , sittin' daining , jiko na stoo, naitakuwa ni selfconted, natarajia pia mnipe ushauri nitafikia wapi?? Wapendwa
 
Mkuu inategemea ukubwa wa nyumba, vyumba na ubora wake. Kuna nyumba ya rafiki yangu nilikuwa naangalia juzi, msingi peke yake umegharimu kama milioni 5, kwa kuwa kiwanja kipo kwenye eneo lenye undongo wa mfinyanzi. Ukiangalia matofali unaona matofali yameshiba kweli, sio yale ya kupukutika ambayo ukijenga leo baada ya miaka kumi yanaanza kupukutika,

Kwa hiyo kimsingi milioni 10 inaweza kutosha kama unataka kujenga nyumba ya mbavu za mbwa, milioni 10 inaweza kutosha nyumba mbili, lakini kama ni nyumba ya kisasa ya karne hii, milioni 10 bado hela ndogo, inaweza kukujengea nyumba nzuri ndogo kwa asilimia 30 au 40 hivi.
 
Itafika mpaka level ya lenta kabla ya kuezeka. Hii ni iwapo hautacomplicate msingi. Ukicomplicate itaishia kwenye msingi tu.
Du! kumbe huyu mdau sometimes anaongeaga fact!! ni kweli kabisa kwa pesa hiyo itafikia hadi kwenye lenta.
 
Nimefurahi sana mada hii kuiona, kwani mm nina m20, mchanga na mawe ya kutosha ninayo, eneo morogoro, room 3 , sittin' daining , jiko na stoo, naitakuwa ni selfconted, natarajia pia mnipe ushauri nitafikia wapi?? Wapendwa
Ukisimamia mwenyewe,yaani uwepo physically,na chenji itabaki kwa pesa hiyo!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Kwa milioni 18 nilizozipataga somewhere, nilifanikiwa kujenga mpaka kuezeka nyumba ya vyumba 4 (viwili vikiwa master rooms), siting & dining room,jiko,store, na study room.

ukipiga ratio hapo! ukijibana na kuwabana sana mafundi unaweza maliza boma lote na kuweka mbao za bati! hela ya bati itabidi utafute.
 
Du! kumbe huyu mdau sometimes anaongeaga fact!! ni kweli kabisa kwa pesa hiyo itafikia hadi kwenye lenta.

yuko poa sana mkuu, sema tu inategemea anaongea akiwa jukwaa gani, huwa unamsikia akiwa siasani nini, teh teh teh!!
 
Ungeweka ramani ya nyumba yako wadau humu watakushauri vizuri zaidi.
 
Back
Top Bottom