Habari wa JF , naomba msaada wa kimawazo na ushauri, Nina Mil.10 ninaplan ya kujenga nyumba yenye vyumba 3,
Je kwa hiyo pesa nyumba yangu itaishia wapi?
Kwa wenye uzoefu wa mambo ya ujenzi tafadhari....
Jenga mkuu, kama kama kiwanja chako kiko kwenye eneo la flat na la kichanga ambalo sio mfinyazi basi kwa kifupingharama zako zitakuwa hivi
Msingi: tofali 500 x 1200tsh= 600000/= msingi wako utakwa wa tofali tano (height)
Cement: msingi 15x17000= 255000
Nondo za mkanda (10 mm) 15x15000=225000
Cement za mkanda 15x 17000 = 255000
binding wire, mbao, misumari, ring, maji na dharura: 500,000/=
Kokoto unanunua mende moja 300000, kokoto zitabakia mingi za kuwekea mkanda wa juu rental
mchanga mende moja 300000
JUMLA YA MSINGI BILA HELA YA FUNDI = 2,455,000/=
Boma: Tofali 1040 x 1200= 1,248,000
Cement 20x 17000= 340000
Mchanga mende2 =600000
Maji na mengineyo= 500,000
JUMLA YA BOMA BILA HELA YA FUNDI = 2,688,000
Mkanda wa juu, hapo inakuwa ni nafuu kidogo kwani mbao utakuwa nazo, kokoto zitakuwepo, mchanga utakuwepo na size yake itakuwa ndogo kwani tofali zitakuwa za wima na gharama yake itakuwa hivi
Nondo (mm10) 15x 15000= 225000
cement za mkanda 15x 17000= 255000
Binding wire, ringi, misumali, mbao za sahani, maji na dharura=500000
JUMLA JUMLA YA MKANDA WA JUU BILA FUNDI = 980000
JUMLA KUU BILA FUNDI = 6,123,000/=
KIFUSI CHA KUJAZA NDANI NA KAZI ZA DHARURA= 2,000,000/
FUNDI MAKUBALIANO LAKINI ISIZIDI = 2,000,000
JUMLA YA MWISHO 10,123,000/=
mimi sio fundi ila nina uzoefu sana wa ujenzi hasa wa Dar,
hiyo gharama imezingatia kuwa , kiwanja chako kiko tambarare, na ground ni ya kichanga au udongo unaofanan na kichanga sio mfinyanzi
pia hesabu hiyo itapatikana tu ikiwa kila kitu unanunua mwenyewe na wewe ndio msimamizi mkuu wa show nzima