Hapo umenena mkuu, kwa maana Thamani ya Nyumba wakati mwingine inategemea na aina ya Nyumba unayotaka kujenga, ya kisasa au Nyumba yenye vyumba tu, je unataka vyumba au sebure zenye ukubwa gani, unataka kupaua au finishing ya aina gani? Hayo maswali yakipata majibu ndipo unaweza kufanya tathimini nzuri zaidi.Ungeweka ramani ya nyumba yako wadau humu watakushauri vizuri zaidi.
Labda kama akiwa huku huwa anabadilika, lakini akiwa kule siasani anajitoa akili kabisa na anatema pumba za kutosha.yuko poa sana mkuu, sema tu inategemea anaongea akiwa jukwaa gani, huwa unamsikia akiwa siasani nini, teh teh teh!!
Ni kweli kabisa mkuu, kwani lengo langu lilikuwa hilo hilo.Hapo umenena mkuu, kwa maana Thamani ya Nyumba wakati mwingine inategemea na aina ya Nyumba unayotaka kujenga, ya kisasa au Nyumba yenye vyumba tu, je unataka vyumba au sebure zenye ukubwa gani, unataka kupaua au finishing ya aina gani? Hayo maswali yakipata majibu ndipo unaweza kufanya tathimini nzuri zaidi.
Labda kama akiwa huku huwa anabadilika, lakini akiwa kule siasani anajitoa akili kabisa na anatema pumba za kutosha.
Itafika mpaka level ya lenta kabla ya kuezeka. Hii ni iwapo hautacomplicate msingi. Ukicomplicate itaishia kwenye msingi tu.
Mkuu inategemea ukubwa wa nyumba, vyumba na ubora wake. Kuna nyumba ya rafiki yangu nilikuwa naangalia juzi, msingi peke yake umegharimu kama milioni 5, kwa kuwa kiwanja kipo kwenye eneo lenye undongo wa mfinyanzi. Ukiangalia matofali unaona matofali yameshiba kweli, sio yale ya kupukutika ambayo ukijenga leo baada ya miaka kumi yanaanza kupukutika,
Kwa hiyo kimsingi milioni 10 inaweza kutosha kama unataka kujenga nyumba ya mbavu za mbwa, milioni 10 inaweza kutosha nyumba mbili, lakini kama ni nyumba ya kisasa ya karne hii, milioni 10 bado hela ndogo, inaweza kukujengea nyumba nzuri ndogo kwa asilimia 30 au 40 hivi.
Habari wa JF , naomba msaada wa kimawazo na ushauri, Nina Mil.10 ninaplan ya kujenga nyumba yenye vyumba 3,
Je kwa hiyo pesa nyumba yangu itaishia wapi?
Kwa wenye uzoefu wa mambo ya ujenzi tafadhari....
acha kudanganya japo hali ya uchumi si nzuri Tz haiwezi kuwa hivyo
Kuna watu mnapenda kila kitu kubishana. Hayo mambo ya jukwaa la siasa. Hili ni jujkwaa lingine. Haya majukwaa yana maana yake.
Unachotakiwa kusema kama unaona nilichosema mimi si sahihi ni wewe kutoa makadirio unayoona sahihi.
Kulingana na uzoefu wangu wa kujenga Dar es Salaam nyumba kadhaa nina uhakika kuwa iwapo msingi hautakuwa complicated na iwapo mdau atasimamia asiibiwe na mafudi, basi pesa hiyo inafikisha lenta kwa nyumba aliyotaja.
Kunä mdau Kituko ameenda mbali zaidi na kupiga mahesabu hatua kwa hatua. Yaangalie mahesabu yake halafu uonyeshe kama kuna kasoro.
Mkuu Kituko kwa mchanganuo mzuri uliotoa, hebu elezea vipimo vya vyumba ulivyotumia ili iwe msaada zaidi!
Ukisimamia mwenyewe,yaani uwepo physically,na chenji itabaki kwa pesa hiyo!
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Ndugu we anza tu mil 10 unajenga mpaka level ya lenta na kubakiwa na vijisent vyako
Jenga mkuu, kama kama kiwanja chako kiko kwenye eneo la flat na la kichanga ambalo sio mfinyazi basi kwa kifupingharama zako zitakuwa hivi
Msingi: tofali 500 x 1200tsh= 600000/= msingi wako utakwa wa tofali tano (height)
Cement: msingi 15x17000= 255000
Nondo za mkanda (10 mm) 15x15000=225000
Cement za mkanda 15x 17000 = 255000
binding wire, mbao, misumari, ring, maji na dharura: 500,000/=
Kokoto unanunua mende moja 300000, kokoto zitabakia mingi za kuwekea mkanda wa juu rental
mchanga mende moja 300000
JUMLA YA MSINGI BILA HELA YA FUNDI = 2,455,000/=
Boma: Tofali 1040 x 1200= 1,248,000
Cement 20x 17000= 340000
Mchanga mende2 =600000
Maji na mengineyo= 500,000
JUMLA YA BOMA BILA HELA YA FUNDI = 2,688,000
Mkanda wa juu, hapo inakuwa ni nafuu kidogo kwani mbao utakuwa nazo, kokoto zitakuwepo, mchanga utakuwepo na size yake itakuwa ndogo kwani tofali zitakuwa za wima na gharama yake itakuwa hivi
Nondo (mm10) 15x 15000= 225000
cement za mkanda 15x 17000= 255000
Binding wire, ringi, misumali, mbao za sahani, maji na dharura=500000
JUMLA JUMLA YA MKANDA WA JUU BILA FUNDI = 980000
JUMLA KUU BILA FUNDI = 6,123,000/=
KIFUSI CHA KUJAZA NDANI NA KAZI ZA DHARURA= 2,000,000/
FUNDI MAKUBALIANO LAKINI ISIZIDI = 2,000,000
JUMLA YA MWISHO 10,123,000/=
mimi sio fundi ila nina uzoefu sana wa ujenzi hasa wa Dar,
hiyo gharama imezingatia kuwa , kiwanja chako kiko tambarare, na ground ni ya kichanga au udongo unaofanan na kichanga sio mfinyanzi
pia hesabu hiyo itapatikana tu ikiwa kila kitu unanunua mwenyewe na wewe ndio msimamizi mkuu wa show nzima
Asante! Hebu nisaidie tena kuanzia hapo ilikofika, mil 10 zingine zitaifikisha wapi?