Nina mil1na nusu je nikinunua hisa za Voda zinaweza nilipa

1,500,000 / 850 * 30 = 52,941/= Approximate dividend ya mwaka.
 
Nimekupata vyema mkuu umefafanua vizuri
 
nunua pikipiki isajili ukishamaliza tafuta mwendeshaji kila siku akupe 6000 badala ya elfu 7 matengenezo yote ni juu ya dereva achana na hio biashara ya hisa nisawa na kulima karanga kwenye shamba la shule
 
Na bado iyo pesa wanakata chini ya 18% ya kodi ya serikali.
Sema kwa wafanyabiashara wanatumia kama dhamana ya kupata mkopo wa haraka. Maana hisa kwa benki ni fasta, kupata mkopo kwa hisa ambazo zipo vizuri sokoni,
 
Kwa kiasi hicho cha hela achana na mahisa. Nenda vijijini chukua mahindi sogeza mjini na uza. Rudia hii kwa muda utaleta mrejesho hapa. Hata pesa ikiwa ngumu vipi watu watakula tu!
 
Hisa ni pasua kichwa,
Jiweke tu huko, kisha ujinyonge kwa kukosa gawio.

Yaani Hisa ni sawa na kulima shamba la miwa jirani na shule (za chekechea , shule za msingi hadi sekondari hadi vyuo vikuu vya Kata ).

Kwa kifupi, Hisa haihitaji uwe na hela za mawazo na kutegemea hiyo hela kuendesha maisha.

Kumbuka, ukisikia kitu unawekeza hela yako, ila bado wanakutahadharisha,,, Eti Vigezo na Masharti Kuzingatiwa,,, ogopa sana hiyo kauli ""

Nitarudi tena ... ... ...
 
Kama ni kijana mpambanaji, bora uiongezee kidogo ununue bodaboda upge nayo kazi mwenyewe.
 
Uwezekano wa kupata faida kwa kampuni kama Vodacom ni mkubwa ila kumbuka kuwa kiuchumi wanahisa huwa hawagawani faida bali gawio hutokana na kitu kinachoitwa DIVIDENDS yaani NYARA na kiwango cha gawiwo kwa msimu mmoja hutegemeana na kiwango cha hiyo nyara kulinganisha na kiwango cha wekezo la hisa zako ktk mtaji wa uendeshaji wa kampuni ndani ya muhula husika. Sasa usishangae mfano baada ya muhula labda wa mwaka kwa hisa zako za thamani ya 1milion ukapata gawio la Tshs 1345.60. Make sense, yaani kwa mwaka ukapata Sh elfu moja mia tatu arobaini na tano na sent sitini. Ndio maana biashara hii inawafaa watu wenye fedha nyingi ambao huwekeza fedha zao za ziada.
 
Nimefaidika sana na hii thread,big up wote mliotusaidia kutoa mawazo,hivyo chukua akili ya kuambiwa changanya na yako.
 
Nimekupata vyema mkuu
 
Kwa uchumi huu,kwanza ulimskia mkuu juz kat anasema anataka aanze na makampun ya sim sasa,kwamba kuna kod nying ilikwepwa.?sasa hyo ni red light mzee,kua macho,usije skia voda wanadaiwa bil400 toka kampun ianze,na ndo utakua mwisho wao..hyo pesa ya dafu naona unataka itupa tuu..tigo juz juz waliwakata watu pesa na hazijarud had leo,ukiwapigia ohh ztarud,..ni red light wadau.si mda mzur huu kununua hisa za any company,..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…