Inawezekana,lakini hela sio rahisi kuiba,nilifanya manunuzi mwenyewe ya kila kitu. Dunia imekuwa kijiji,fundi alikuwa akinipa mahitaji ya Rangi nawasiliana na mafundi wengine wanipe makadirio yao,mara nyingi yalikuwa yanacheza mule mule,nikijiridhisha naweka oda kiwandani mzigo ukiwa tayari unaenda Site. Nimefanya hivyo kwa kila kitu,kuanzia Bati,tiles,Vifaa vya umeme,vifaa vya mabomba, Aluminium n.k...
Nilitaka kuleta uzi humu kuwaambia watu Dunia imekuwa kijiji sa hivi,mfano tiles fundi alinipa vipimo vyake,nikatuma kwa jamaa yangu Engineer akasema viko sawa,Ishu ilikuwa kwenye bei,nilitafuta namba za Twyford kwenye website,nikawapigia wakanipa namba za wakala wao aliye jirani na site,nikaweka oda kisha nikamwambia fundi akakague,akasema ziko sawa,mzigo ukaenda Site. Nimefanya hivyo kwa kila kitu.Kitu pekee ambacho nahisi kupigwa ni cement na Tofali...maana walikuwa wanatoka nje ya hesabu wanazonipa wanaomba nyongeza.