Nina milion 10 nahitaji kujenga nyumba Mwanza

Kama uko mbali na site kuibiwa kupo mkuu.

Yawezekana 20+ imepigwa au zaidi hali ni mbaya sana mafundi na hata watu wengine siyo waaminifu hapo unakuta wameiba material na hela.
Ujenzi ni gharama sana mkuu,kama jamaa hapo juu anakwambia katumia mil 23 ndio kwana anapaua na kasimamia kila kitu. Hapo ndio ujenzi unaanza aandae milion 50 nyingine.
 
njoo nikupe kiwanja
 
Ni kweli mkuu kwenye cement hapo siyo rahisi kuwazuia kuiba maana wanaweza kuiba hata mchanga uliochanganywa na cement wakauza, hata tofari ni hivyo hivyo.
 
Ujenzi ni gharama sana mkuu,kama jamaa hapo juu anakwambia katumia mil 23 ndio kwana anapaua na kasimamia kila kitu. Hapo ndio ujenzi unaanza aandae milion 50 nyingine.
Hata mimi niko hatua za kupaua nimeshatoboka 16 tayari.
 
Ni kweli mkuu kwenye cement hapo siyo rahisi kuwazuia kuiba maana wanaweza kuiba hata mchanga uliochanganywa na cement wakauza, hata tofari ni hivyo hivyo.
Yeah kweli Cement inawezekana waliiba lakini walikuwa wanajitetea,wanasema kiwanja kina slope kwahiyo Tofali zimeenda nyingi,na msingi waliochimba wanasema mtu alikuwa anazama haonekani,nyumba imenyanyuka juu balaa.Nilielewa.
 
Hata mimi niko hatua za kupaua nimeshatoboka 16 tayari.
Hapo ndio ujenzi unaanza mkuu,ila gharama za kutoka hapo na kuendelea inategemea na wewe ni muumini wa brand ama la. Kama mie kila kitu niliweka brand,bati nilipiga ALAF,rangi PLASCONE, tiles TYWFORD ,vifaa vya plumbing na masink nilichukua twyford pia,kwahiyo gharama huwa zinatofautiana kulingana na brand unazochagua,ukichukua brand cheap utamaliza nyumba kwa hela ndogo.
 
Kama uko mbali na site kuibiwa kupo mkuu.

Yawezekana 20+ imepigwa au zaidi hali ni mbaya sana mafundi na hata watu wengine siyo waaminifu hapo unakuta wameiba material na hela.

Mmm hawez kupigwa kiasi chote hicho mkuu kwenye 70m ndo tunasema Hamna uzoefu mnatisha tu watu
 
Ujenzi wa mbali tunaibiwa sana. Miaka ya nyuma nilifanya ujenzi Morogoro nikiwa naishi Arusha, nyumba ya 75m zilitumika zaidi ya mia. Hata ukinunua materials yote,wanaiba na kuyauza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…