Nina milioni 20. Nahitaji kufanya biashara ya spare za pikipiki kwa jumla na rejareja

Kweni ukienda kuchukua china hutajirishi mtu?Milioni 20 hela ndogo sana kwa kuanza biashara ya import tena ambayo huna uzoefu nayo.Unachotakiwa kuanya kwanza ni kutafiti bei za bidhaa kwa hapa nchini,kisha ulinganishe na bei ya kule uchina,kisha unagalie na gharama nyingine uone kama katika hio 20 Milioni namna bora ni ipi.

Huo ni ushauri wangu kwako. Iwapo unahitaji msaada zaidi katika mchakato mzima wa kutafuta taarifa za bei za bidhaa za duka la pikipiki kwa hapa Bongo pamoja na kula uchina pamoja na fursa nyingine na changamoto basi tuwasiliane zaidi.

Karibu
 
Ni biashara yenye kuzaa mara 2

Nunua mzigo tz....peleka site.....tafuta mafundi wazuri na waaminifu watakuuzia spare zako vyema.

Uza spare original....duka lako litapata jina zuri.
Jitahidi pikipiki uifahamu usiwaache mafundi kila kitu wanaweza kukugombanisha na wateja.
Mfano fundi anaweza kusema chukua spare hii...tatizo litaisha....anafunga halafu bado...inabidi mteja anunue nyingine tena. Hii itasababisha kuonekana unajali tuu uuze spare.
Wape mafundi ushauri
 
Hivi hii biashara unaweza pata 200K kwasiku ??

Portfolio | 2020

Kikawaida biashara yeyote inaweza kuingiza kiasi hiko au hata zaidi mkuu! Issue ni wewe mfanyabiashara, uweke mbinu itakayokufikisha hapo kwenye 200k


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Mkuu
Ushauri wangu andaa list ya vitu unavyotaka kwenda kununua China then pita kkoo jua bei zake za jumla.
Baada ya hapo andaa Safari, ila subiri Corona apite kwanza,
Pia nauli hata iwe high season huwa haizidi 1400 USD. Labda kama utataka kukata Busness class
Hiyo hela inatosha kwa kuanzia ila ujue nini cha kununua, jitahidi sana kujua walaji wako wanataka nini,
Fanya maamuzi ,hutajutia,
 
Nakuunga mkono kamanda..!
 

Shukran sana mkuu kwa maoni, mawazo... Ndio maana kabla sijakurupuka nikaona nije hapa jamvini nikiamini nitapata chochote chakunipa mwanga, na ni kweli kea hizi comments napata mengi kuliko nilivyotaraji. SHUKRAANI

Sasa mkuu wangu... kulingana na hii comment yako inaonesha wewe umeshafanya hizi biashara za china au una mtu wako wa karibu anaefanya, ndio maana umecomment kitu kilichoingia deeply kidogo.

Ok sasa hebu fanya kama mimi mtoto wako... Nipe ushauri kutokana na uzoefu wako, kulingana na huu mtaji wangu nifanye kipi unachoona kitafaa kati ya hivi :-

• Kununua kariakoo
• Kwenda china

Kama ni kwenda kariakoo Hakikisha jibu lime base kwenye mtaji wa mil 20...

Kama ni kwenda china jibu pia liwe kwenye mtaji wa mil 20, pia unaweza kuongezea nyama hapa hasa kwenye suala la connections ili kumalizana na wale TRA katika hali ya mtaji wa mil 20.

Mkuu hata ukishindwa kumwaga hapa naomba hata DM mkuu, nitatoa hata ya maji 🤝


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Mkuu kuhusu mtu wa kuweka nae kwenye behewa hilo tatizo lilikiwepo miaka ya nyuma sana huko, kwa sasa kunamakampuni ya kitanzania yamefungua ofisi China, kama(Tosh cargo)(Silent Ocean)(Moka) na wengineo.

Mteja unapeleka mzigo,wako wanaupima ujazo mnajaza form yenye maelezo ulichopakia na ukubwa wa mzigo,wanakupa copy yako ,wewe unaondoka zako kurudi bongo.

Mzigo ukifika wanakupigia simu una kwenda ofisini kwao unalipia unachukua mzigo wako
 

Umewahi kufanya biashara za China mkuu?
Tujitahidi kushauri kile tunachokijua vizuri,
Tukiona kitu hatukijui tuwe tunapita kusoma comments tu, sio lazima tuchangie kila kitu,
JF imesaidia wengi sana, sasa tusiwakatishe watu tamaa watu kwa vitu ambavyo hata sisi wenyewe hatuvijui.
 

Shukraani mkuu... Kuhusu ngeli niko daraja moja na SHISHI [emoji1]! Sema nini kamanda, nchi ya kibiashara kama china kwenye suala la mawasiliano wala sii ishu kubwa, maana kule kuna muingiliano wa wafanyabiashara kutoka mataifa yote dunuani.. Na sio kila mmoja anaweza kingeli, sasa kutokana na hilo basi maeneo ya kibiasha lazima huwa na lugha ya ishara! Yaani unaweza kuwasiliana bila kutoa sauti, ukaongea kwa mdomo bila sauti huku ukifuatisha kwa mikono, lazima muelewane..

Ukiamua unaweza kuweka APP ya translation kwenye simu, Mambo yakaenda..

Shukraani mkuu




Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu kwanza nikupe hongera kwa kuweza kutengeneza kiasi hicho cha pesa japokuwa hujasema kwa sasa unafanya nini,mim nikushauri tu kwamba kama alivyoshauri hapo juu ni kwamba biashara sio hela tu ni zaidi ya pesa na wataalam wa biashara wanasema ujuzi wa biashara ndio mtaji mkubwa zaid kuliko pesa hivyo anza kwanza kupata ujuzi kabla ya kufikiria kwenda china kwani hii ni kutaka kuanzia juu wakat biashara huwa inaanzia chini.

Ni kweli biashara ya spare za pikipiki zinalipa kwa sasa hivi sema hii corona virus imekuwa ni tatizo na bado hatujui itaisha lini. Kama alivyoshauri mkuu mmoja hapo juu chukua kiasi kidogo kama 5m fungua duka la reja reja fanya kazi kupitia hilo utajua aina za pikipiki na spare zake na zile ambazo mahitaji ya spare zake yapo juu kuliko zingine na utawajua wauzaji wa jumla kwa kariakoo sasa kadri utakavyokuwa unafnya utazidi kupata ujuzi na taarifa muhimu zaidi kuhusu hii biashara na kitafika kipindi utajiona tu sasa unatosha kwenda china na hapo taarifa nyingi utakuwa nazo.

Nasisitiza tena ukianza biashara bila ujuzi yaani "Technical know how " utapoteza pesa yote na hutafikia lengo ndio kuna mkuu moja amekuambia hiyo pesa ni peanut ni kweli ukiwaza kwenda kufunga container na 20m ni peanut lakin ukiwaza kwa upande wa pili ni pesa nyingi. Kuna mkuu mmoja aliwahi kuleta uzi mmoja humu kuhusu biashara ya China na Tanzania ule uzi una vitu vingi sana kuhusu safari, clearing , TRA na vinginevyo vingi tu utafute usome ukiwa umetulia utajifunza mambo mengi kuhusu biashara ya China na Tanzania nafikiri mkuu alotuma huo uzi anaitwa kipilipili utafute usome ukiwa umetulia.

Mwisho nikutakie kila la kheri.
 

Dah mkuu kama najaribu kukupata hivi, Yaani kama inakuja inakataa hivi...


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Shukraani sana mkuu... Ngoja nijongee PM


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Ushauri wako nimekuelewa sana mkuu.. Alafu inavyoonekana kama funfi ndie anaekuuzia spare mkuu! Upa kuna strategy nimei note kichwani aisee


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Silent ocean niliulizia gharama zao 1 cubic metre USD 450, pamoja na kutoa mzigo bandarini.

Samahani mkuu..1 cubic metre unamaanisha kipimo gani? Sijaelewa hapa..


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nami nina ushauri kidogo mkuu.

20 mil tuu hata kwa kwenda kununua nguo tuu china ni ndogo sana sembuse spare za pikipiki? Yes, ni kweli inalipa. Lakini kila kitu ninconnections mkuu. Usione business ya mtu inaenda poa ukadhani mambo ni rahisi. Ngumu mno. Nakushauri anzia mtaani. Fanya rejareja na usiweke pesa yote. Talking from experience.

Kama una jamaa yako unamjua na munaaminiana basi orodhesha list ya bidhaa inazohitaji akisafiri akununulie na vyako aweke kwenye kontena lake. Wanaoenda nunua spare nje wanatumia pesa ndefu sana. Tofauti na ukaanza kidogo ili kuboost biashara yako.

Pia unapaswa kujua ni spare zipi demand yake ni kubwa sana na ni za aina gani ya pikipiki. Sikushauri uende china utalua kwa pesa hiyo. Mbona hawa wa maduka ya mtaani walianza kwa kununulia kkoo and now wako na multiple shops na wanasafiri? Usiogope. Anza sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…