GREAT INVESTOR
Senior Member
- Nov 13, 2018
- 128
- 297
Habari wanajukwaa.
Ee Bwana ee, nimekuja kwenu wana jukwaa, kuomba tusaidiane mawazo kama kichwa cha habari kinavyosomeka.
Baada ya kumaliza chuo 2019, Mungu alinifungulia mlango nikapata kazi ya miaka miwili na NGO x hapa Nchini, kutokana na msoto uliopo kitaa niliona ni vyema nijibane niweze kusave pesa walau nifanye kitu kitakacho nisaidia. Mkataba wangu umefika tamati na namshukuru Mungu nimeweza kusave takribani milion 22.
Nilikuwa na mawazo mawili, la kwanza ni kujenga nyumba kwa kuwa nilishanunua kiwanja.
La pili, ni kufanya biashara, ila kwa bahati mbaya bado sijawa na wazo zuri la biashara.
Naombeni mawazo yenu, nijenge au nifanye biashara, kama ni biashara Je, unahisi biashara gani nzuri katika mkoa wa Arusha?
========
Baadhi ya mawazo ya wadau
Pia soma: Nina mtaji wa Milioni 35 nataka kufanya biashara Kariakoo

Mkuu, 22Mil, sio haba na sio nyingi. Aina ya biashara inategemea ulipo, interest zako, life style yako na malengo yako. Kwa ujumla inakubidi kwanza utulie uiweke hela yako kwenye FIXED DEPOSIT na kisha uanze sasa kujenga wazo la biashara.
Katika kutafiti wazo la biashara hakikisha unazingatia kutumia wataalamu ili kupata picha kamili ya aina ya biashara unayofikiri kufanya .Kuna aina nyingi za biashara unazoweza kufanya ila jambo la muhimu ni kuwa innovative ili uweze kuleta ushindani. Hilo ni muhimu sana.
Usishawishike kufanya biashara bila kuwa na taarifa sahihi kwani hatari yake ni wewe kupoteza na kukata tamaa.
Wewe fanya mpango ujenge ila nyumba iwe nzuri hata ukiweza kupangisha kwa familia moja iwezekane, biashara sasa hivi hazieleweki na pia ukijenga pesa ya biashara huwa tunakutana nazo tena ila hela ya kujenga ukafanya biashara kipindi hiki ambacho hakieleweki kabisaa utabaki na picha ya nyumba kwenye kichwa maana biashara inataka utulivu wa kichwa na pia usitafute biashara za haraka ili ujenge daah.
Pia soma: Nina mtaji wa Milioni 35 nataka kufanya biashara Kariakoo