Habari wanajukwaa.
Ee Bwana ee, nimekuja kwenu wana jukwaa, kuomba tusaidiane mawazo kama kichwa cha habari kinavyosomeka.
Baada ya kumaliza chuo 2019, Mungu alinifungulia mlango nikapata kazi ya miaka miwili na NGO x hapa Nchini, kutokana na msoto uliopo kitaa niliona ni vyema nijibane niweze kusave pesa walau nifanye kitu kitakacho nisaidia. Mkataba wangu umefika tamati na namshukuru Mungu nimeweza kusave takribani milion 22.
Nilikuwa na mawazo mawili, la kwanza ni kujenga nyumba kwa kuwa nilishanunua kiwanja.
La pili, ni kufanya biashara, ila kwa bahati mbaya bado sijawa na wazo zuri la biashara.
Naombeni mawazo yenu, nijenge au nifanye biashara, kama ni biashara Je, unahisi biashara gani nzuri katika mkoa wa Arusha?
========
Baadhi ya mawazo ya wadau
Pia soma: Nina mtaji wa Milioni 35 nataka kufanya biashara Kariakoo