Nina Milioni 45, msaada wanaJF

Milioni 45 ushindwe kujenga na kumaliza?

Unaweza nunua hata pagala kuna mapagala unanunua 20 unatumia million 10 kumalizia..

Naona wewe ulivyojenga mwanzo ulipigwa Sana na mafundi..
Hapana ndugu kwa sahivi swala la ujenzi tunataka kuliweka pembeni tutakachozalisha kutokana na biashara tunaweza kukitumia kujengea uku mtaji ukiwa unaendelea kupumua maana kwenye ujenzi siku zote ni kutoa tu wala sio kuingiza ndugu ni sawa na mshahara wa sisi waajiriwa tunatoa tu hakuna backup
 
Namtakia mafanikio mema lakini kuna kila dalili ya mtu kulizwa hizo fedha hata kabla hajaanza biashara. Dalili zote zinaonyesha hivyo. Kweli dunia ya leo unaonyesha nyama uliyobeba kwenye kundi lenye mafisi?

Hata kama hatalizwa (tena na member(s) kutoka hapa hapa) akifanya biashara uwezekeno wa kufanikiwa ni mdogo.

kisumapai ni bora kama huna wazo lolote kwa sasa basi chukuwa fedha zote, tafuta benki yenye riba nzuri, weka fixed kwa muda wa mwaka au miezi sita, ili upate muda wa ku-research utafazifanyia nini.
 
POLE SANA, Nakuomba sana hiyo pesa irudishe bank au kwa hao waliokukopesha haraka, Pesa ngeni, kazi ngeni , wewe mgeni kwa hakika hiyo ni BALAA, Pesa bila PLAN ni balaa..
Sio kila pesa ni neema inategemea umeipataje na uzoefu nayo na uzoefu wa kazi yake pia n.k,,,

Mimi ni mjasriamali pia tena mzoefu kiasi changu, kwa miaka hii ya karibuni tena kwa shughuli za kuchanganya mikono ya watu au kutumia watu, HAKIKA HAKUNA BIASHARA YA MKOPO 100% ITAKULIPA tegemea maumivu na hasara kubwa BORA UZIRUDISHE HIZO PESA.

Bank au mikopo mingi Riba ni kuanzia 18% na kuendelea na biashara nyingi zinazolipa sana
zinazosifiwa huishia 8% hadi 13% kwa mwaka baada ya kuondoa gharama zote, fatilia
sasa wewe ukodi pesa kwa 20% mfano na zikuzalishie 12% UTAPONA ? ?

Aidha uwe tayari kujifunza biashara/ujasriamali kabla ya kustaafu kwa KUZIPOTEZA HIZO 45 mln na zinaweza kuisha na usielewe chochote ukaambulia kuchanganyikiwa - BAHATISHA

Nikiwa mjasriamali ni DHAMBI SANA KUMKATISHA TAMAA Mjasriamali anayeanza.

Ushauri wangu anza kidogo kidogo bila mkopo au 30/70 mtaji yaani mkopo 30% isizidi kwa mtaji mali yako iwe 70% ukijiwekea malengo makubwa hata kama utaanzia Sh 5mln tu huko 45 mln utafika tena salama na ari nzr na zaidi,

Washauri wamejaa kila aina ya biashara kwa mitazamo yao TATIZO hawana takwimu linganishi za kukusaidia kuamua badala yake sawa na chukua 45mln ukacheze kamali..
 
Nashukuru kwa ushauri wako ngoja namimi niendelee kupambanua kupitia jukwaa ili maana nimeisha jifunza mengi naona kuna Fulsa nyingi lazima ntaona zile ambazo naweza kupambana nazo kutokana na kazi ninayoifanya na mda ntakaokuwa na upata ila nimejifunza kitu kikubwa kumbe ukitaka kufanikiwa kwenye biashara lazima upambane mwenyewe ndo maana waliopata ndo wale wale.
 
Ushauri BORA sana tatizo bado itakatika sababu mkopo 20% FDR ya juu 11%
 
Asante kwa ushauri ndugu je kwanini usinipe idea ya kufanya chochote ambacho unaona kinaweza kunikomboa kuliko kurudisha pesa je kama nikiendelea kuogopa angali bado kijana je siku watoto wangu wakishindwa kwenda shule kwa sababu ya kipato kidogo ninachokitegemea je hapo ntakuwa nimejikomboa?
 
Naomba nami nitupie cent zangu kama mbili.

1. Kwa hela hiyo fikiria asilimia 20% to 25% au robo uiweke kwenye fixed income investment yaani kitu ambacho kitakuba hela bila kujali kuna hali gani ya corona iliyodhibitika na imehakikishwa. Vitu kama Fixed deposit katika bank ambazo zina rate nzuri kwa , kwenye T. bond na T, bill kila wiki angalia hata za siku 35, 91 na 180 unaweza kupata za rate nzuri kwa mwezi hasa katika mwaka huu wa uchaguzi rate huwa zinakuwa nzuri kwenye hii minada kila wiki inaendeshwa na BOT.

2. Tafuta mradi utakaoleta hela kila siku ili upate kwanza hela la kurudisha makato na maisha yaendelee kaa chini angalie kitu gani unakipenda na unakiweza ambacho kinaweza kukupa hela kila siku fanya hicho maana tumeumbwa kutatua tatizo fulani duniani na moja ya kugundua kitu ulichoumbiwa kukitatua inaweza kuwa ni kitu unachokipenda sana au kitu ambacho unachukia kuona kimefanywa vibaya unakuwa umeumbwa kukitengeneza kikae vizuri.

3. Tafuta kitu ambacho kiko trends ila ambacho wewe unaweza kupita kila siku atleast wakati unarudi jioni MPesa, Tigo pesa, Wakala wa benki zote mjini ya crdb, NMB, Equity, iweke unique kidogo, Kuuza vitu vidogo vidogo vitu kama simu, uwakala wa Bima na biashara zote za mambo ya fedha.
4. Pata utulivu sana isitoke hela ambayo haitakuwa inarudi wa usichuke risk ambazo hazina faida ya moja kwa moja
 
Ushauri BORA sana tatizo bado itakatika sababu mkopo 20% FDR ya juu 11%
Ni kweli mkuu ila nimeona jamaa ana kiherehere sana. Ni bora nusu shari kuliko shari kamili. Kosa kubwa alilofanya ni kuchukuwa mkopo bila kuwa na plan au uzoefu wa biashara. Asipokuwa makini anapigwa hapa hapa na hatajua amepigwaje.

Ni kosa sana kutangaza una fedha kiasi fulani, na unataka kuzifanyia shughuli ambayo huna uzoefu nayo. Labda anaona kwa sababu hapa username yake haiwezi kumtambulisha lakini nimeshaona dalili ya watu kufukizia.

Ni watu walivyo wajanja watamlanisha kidogo kidogo mpaka aingie kingi, wapige. Naanza kuona dalili ya watu kujitolea hata kupoteza milioni kadhaa ili wamweke sawa aingie kingi.
 
Huyu ataweza hata kuzipeleka kanisani ba mchungaji akaziombee na akaziacha huko huku akilipa marejesho..

Yaani ni kosa la jinai, kuchukua hela halafu ukawa hujui unataka kuzifanyia nini..
Hawajui hela ni shwetani, zitapata misiba, ugonjwa, ada za ndugu wasioeleweka, wapigaji wa mitaani wenye deals too good to be true, MR KuKu, D9, DECI..akija kushtuka madalali wanapaka rangi nyumba inauzwa..

Simuombei mabaya ila planning ni muhimu SANA katika maisha haswa ya biashara, usikurupuke!

Everyday is Saturday.........................😎
 
Kwasababu hukujiandaa kuchukua mkopo nunua Jenga nyumba nyingine weka wapangaji my friend. Hizo business ulizozitaja inabidi angalau uwe experienced kidogo
 
Asante kwa ushauri ndugu hakika mawazo yako ntayafanyia kazi japo kuna neno moja umelitumia la kusema nina kiherehere usijal kuhusu ilo pia iyo ni njia ya kufikisha ujumbe ili uwe na uzito fulani
 
Kwasababu hukujiandaa kuchukua mkopo nunua Jenga nyumba nyingine weka wapangaji my friend. Hizo business ulizozitaja inabidi angalau uwe experienced kidogo
Asante kwa ushauri ntakupa mrejesho ndugu
 
Angalizo kwenye hii biashara ya mpunga.

Ni kweli kabisa kwa mahesabu uliyompigia sehemu nyingi ununuzi wa mpunga uko hivyo na siku hizi kila eneo linalolimwa mpunga kuna dalali (sijui kama ni kote ila Morogoro sehemu nyingi wapo) ambapo bila huyo inakuwa changamoto kupata mpunga

Chakufanya ni kutenga muda kuzunguka na huyo dalali ili ujihakikishie upimaji na aina ya mpunga ili kuepuka kununua mpunga mbaya na kupunja kwenye upimaji

Pili ni vizuri kuwa makini kuchagua sehemu ya kutunzia maana baadhi ya magodauni kuna wafanyakazi wasio waaminifu siku ya kuja kuuza mpunga wako kupoteza gunia tano na kuendelea ni kawaida halafu mnarudi kusumbuana kwenye kudaiana

Tatu, wanunuzi wengi wa mpunga uliotunzwa stoo wanalazimisha kununua kwa kilo wakati wewe ulinunua kwa kupima kwa ndoo, hapa mara nyingi inakula kwako maana kwenye zile ndoo mara nyingi kilo hazitoshi hivyo ni vizuri wakati wa kuuza ukoboe uuze mchele

Na mwisho kabisa mpunga ukishafika elfu 60 kwa gunia ukijumlisha na hizo gharama nyingine inafika hadi elfu 71 au elfu 72 usijisumbue kununua labda kama unatunza fedha maana mara nyingi mpunga unaishia elfu 90 au laki moja lakini kwa kupima kwenye mzani ambapo hata kwa dawa gunia moja halitimii

Pamoja na yote hayo biashara ya mpunga ni ngumu kupata hasara ya kupoteza mtaji wote. Utarudisha hela au utapoteza kidogo kama soko litakuwa baya hasa hasa kwa miaka ya hivi karibuni ambapo Tanzania inazuia kuuza chakula nje

Kwa vile yuko DSM afanye survey ya maeneo wanakotunza mpunga na wanunuzi hasa wa kutoka nje wanaenda kununua pale kisha ajisogeze Morogoro maeneo ya dakawa au ifakara kupeleka dsm sio mbali sana japo anaweza kutunzia huko huko
 
Sio bongo hii....africa bila kusimamia kitu chako mwenyewe au kama huna uzoefu nacho basi we subiri maumivu au kama ukifanikiwa shukuru Mungu.
Hapo hapo unatoa njia ya kufanya , hapo hapo unasema haiwezekani.. confused mind
 
Fanya na ww kuchangia basi tusimjazie jamaa comments nyingi.embu changia na ww nikusikilize pia...ndo maana tupo hapa.mtu akikosea unatoa solution hamna mtu alizaliwa akajua kila kitu bro.
Akija mlengwa ndo akosoe na achuje
Hapo hapo unatoa njia ya kufanya , hapo hapo unasema haiwezekani.. confused mind
 
Nunua tata mpya lipia sumatra weka barabaran tafuta dereva mzoefu piga kazi....kwa siku hukosi 80....ngariba haogopi mikojo wanaoogopa biashara ya abiria na gari walinunua gari mbovu....

Ungekuwa uko free ungechukua ya mizigo cantre uingie mikoa ya uzalishaji wa mazao hukosi hela ila unatakiwa uwe na moyo wa kitajiri hesabu unayoletewa ni sawa na pasu ya dereva na konda....yaani ukiletewa laki ni laki mbili zilipatikana....piga kazi...
 
Nimekuelewa vema, vigezo vya mafanikio ya ujasriamali ni vingi na hasa inategemea na mhusika mwenyawe(management, skills, knowledge etc) mazingira (fursa, rasilimali-mtaji,vitendeakazi, n.k)

Na kwa ufupi Biashara aiza zote zinaweza kumlipa Mr A na hizo hizo Zikamfilisi Mr B, yaani inategemea na vigezo husika, CHAGUA BIASHARA YEYOTE UNAYOONA WEWE INAKUFAA NA INAIPENDA ANZA NAYO MDOGO MDOGO HAKIKA UTAFANIKIWA- UBARIKIWE NA KILA LA HERI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…