Nina Milioni 45, msaada wanaJF

Nina Milioni 45, msaada wanaJF

@kisumapai
Nimesoma kwa utulivu ulichokiandika na nimeona haya
1. Katika siku 30, Mshahara wako na mwenza wako unatosha kwa siku kadhaa (tarehe 14 huwa hamna fedha za kutosha).
2. Hamna uzoefu wa biashara.
3. Umesha shauriana na mwenza wako aina za biashara.
Kwa mtazamo wangu fedha igawanye katika namna hii;
1. Biashara A. Hii iwe biashara ambayo itakupatia pesa ya kusaidia kuwezesha matumizi ya familia yako ya kila siku. Hii biashara iwe na uwezo wa kuingiza pesa ambayo ukiichukua haiwezi kuathiri biashara yenyewe.
2. Biashara B. Hii iwe biashara inayoingiza pesa itakayokuwa inahifadhiwa kama kukuza mtaji wenu wa biashara. Hii biashara iwe na uwezo wa kuingiza pesa kwa mwezi angalau faida ya asilimia 30% ya mtaji ulio wekewa (baada ya kutoa garama zote).
3. Biashara C. Hii iwe biashara ambayo itaweza kuingiza faida ya angalau 50% ya mtaji kwa kipindi cha kuanzia miezi mitano hadi nane au mwaka na iwe biashara ambayo unaweza kurudisha faida uliopata na kuongeza kama mtaji na kuipanua biashara hiyo.
Sasa aina gani ya biashara itakua ni biashara A, B na C inategemeana na vitu hivi;
1. Eneo unaloishi au utakalo amua kufanyia biashara
2. Muda utakao kuwa katika usimamizi na uangalizi wa biashara
3. Ujuzi juu ya usimamizi wa biashara ama kuwepo mtu wa kuweza kuangalia taarifa za biashara yako na kuweza kujua mwelekeo wake na kuweza kukushauri nini cha kufanya (iwapo mwelekeo hasi unatokea)
4. Utayari wa kupoteza mtaji (aidha kiasi ama wote).

Biashara inamengi huwezi kuwekeza leo kesho upate faida zingatia hilo na pili kuna tofauti ya mauzo (au pato kutoka kwenye biashara) na faida ya biashara.
Mtu hajawahi kufanya biashara,
afu ndo aanze na utitiri wa biashara.

Tena Ela yenyewe ya mkopo.

Duh! Wallahi mtaita ambyulensi presha itakapopanda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzidi kuajiriwa tu 9am-5pm...
Kama ni kweli, nyie siyo wajasiriamali...haiingii akilini, vichwa viwili mume na mke mchukue mkopo halafu kama mazuzu hamjui nini mnataka kufanya..
Mzitoe hizo hela benki mlale nazo kitandani!

Everyday is Saturday.......................... 😎
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nunua shamba panda miti hata zikiisha zitaonekana zilifanya nini na watoto wako watakuja kuishi maisha ya ukwasi bila nguvu nyingi.
 
Gunia la mpunga hivi sasa ni 42000 anaekununulia anakula 2000 kwakila gunia pia ushuru kila gunia1500 usafiri kwakila gunia kutoa porin hadi stoo2000 vibega kupakia na kushusha1000 mfuko wakuhifadhia tsh800 wafuata mpunga polini ndani ndani kila gunia1000 kuhifadhi stoo1500 kwaiyo gharama zote pamoja ununuzi gunia litakua ni 51800 utakuja kuuza kila gunia ifikikapo december kwa kima cha chini soko likiwa baya utauz tsh 80000 kwaiyo utakua na faida ya tsh 28200 kwa kila gunia.ila ukitaka usiuze mpunga uje uuze mchele yaan ukoboe huo mpunga uwauzie walanguz wa mchele wanaotaka dar uganda nakwingneko gharama itaongezeka kwenye kukoboa ambayo kila kilo utakobolea tsh50 kwaiyo gunia la kilo tisini utalikoboa kwa tsh3000 hapo mchele bei ya jumla utakuta imefika 1700 kwaiyo utazidisha mara kilo60 kila gunia ndo litao hizo kilo za mchele kwaiyo utapata faida ya tsh 47200 sasa zidisha mara gunia utakazo kua na zo stoo utaona faida kias gani umepata ndani ya miez isiyo zidi 10
Ushaur mzuri, ila Tatizo lenu hamuwaambiagi na changamoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
POLE SANA, Nakuomba sana hiyo pesa irudishe bank au kwa hao waliokukopesha haraka, Pesa ngeni, kazi ngeni , wewe mgeni kwa hakika hiyo ni BALAA, Pesa bila PLAN ni balaa..
Sio kila pesa ni neema inategemea umeipataje na uzoefu nayo na uzoefu wa kazi yake pia n.k,,,

Mimi ni mjasriamali pia tena mzoefu kiasi changu, kwa miaka hii ya karibuni tena kwa shughuli za kuchanganya mikono ya watu au kutumia watu, HAKIKA HAKUNA BIASHARA YA MKOPO 100% ITAKULIPA tegemea maumivu na hasara kubwa BORA UZIRUDISHE HIZO PESA.

Bank au mikopo mingi Riba ni kuanzia 18% na kuendelea na biashara nyingi zinazolipa sana
zinazosifiwa huishia 8% hadi 13% kwa mwaka baada ya kuondoa gharama zote, fatilia
sasa wewe ukodi pesa kwa 20% mfano na zikuzalishie 12% UTAPONA ? ?

Aidha uwe tayari kujifunza biashara/ujasriamali kabla ya kustaafu kwa KUZIPOTEZA HIZO 45 mln na zinaweza kuisha na usielewe chochote ukaambulia kuchanganyikiwa - BAHATISHA

Nikiwa mjasriamali ni DHAMBI SANA KUMKATISHA TAMAA Mjasriamali anayeanza.

Ushauri wangu anza kidogo kidogo bila mkopo au 30/70 mtaji yaani mkopo 30% isizidi kwa mtaji mali yako iwe 70% ukijiwekea malengo makubwa hata kama utaanzia Sh 5mln tu huko 45 mln utafika tena salama na ari nzr na zaidi,

Washauri wamejaa kila aina ya biashara kwa mitazamo yao TATIZO hawana takwimu linganishi za kukusaidia kuamua badala yake sawa na chukua 45mln ukacheze kamali..
Chukua huu ushauri mtoa mada[emoji115]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uje kuvuna baada ya miaka kumi na tano....hiyo inahitaji mtu mwenye hela ambayo ni ya akiba na sio ya mkopo
Nunua shamba panda miti hata zikiisha zitaonekana zilifanya nini na watoto wako watakuja kuishi maisha ya ukwasi bila nguvu nyingi.
 
Sio uchawi, lakini naona ukienda kuanguka.
Mmechukua mkopo bila kuwa na plan.
Halafu ni risk sana kuanzisha biashara kwa kuutegemea mkopo 100℅

Mna uzoefu na biashara gani?
Kwa usalama wa hiyo pesa kama una kiwanja ni heri ujengee nyumba upangishe.

Neno langu si sheria. Zaidi labda wataalamu waje
Uko sahihi brother...mkopo si wakuanzishia biashara kamwe, mkopo huwa ni wa kuendelezea biashara!
 
Mimi pamoja na mke wangu ni watumishi wa serikali tumekaa pamoja tumeshauliana tumeamua kuchukua mkopo wa mil 45 lakini tatizo tulilonalo hatuna idea yoyote ya biashara maana kazini tunaenda asubuhi na kurudi jioni.

Japo mungu ametujalia tumeweza kujikwamua na kujenga nyumba ya kuishi maeneo ya boko chasimba.

Shida yangu kwenu je ni biashara gani naweza kufanya ili tuweze kujipatia kipato cha ziada bila kuaribu utaratibu wa kazi maana ikifika tarehe 14 wote tunakuwa tumeishiwa tunabakia ndani kuangalia CD za kikorea na kijapani.
Mawazo niliyokuwa nayo ni÷

1. Ninunue daladala ya habiria.
2. Ninunue bodaboda 5
3. Ninunue bajaji mbili
4. Nifuge kuku wa nyama

Maana siwezi kuweka fixed account kwakuwa pesa yenyew ni ya mkopo ushauri wenu ndugu zangu lakini wazo la daladala ndo tumelipa kipau mbele kikubwa naomba kwa mwenyewe uzoefu na iyo biashara ya daladala anipe msaada kwa umakini maana makato ya miaka 5 sio powa kabisa

Kila mtu anakimbilia biashara ya kuku
Wacha uingie uone changamoto zake
 
Wekeza kwenye Carwash ya kisasa.

Tafuta Location
Mikocheni warioba, Sinza Bamaga, Sinza Palestina, Kinonondoni Morroco-Mkwajuni, Sayansi.

Kwanini CARWASH
1)Sustainable; Siku zinavyoenda ndivyo Soko linapanuka ratio ya ununuzi wa vyombo vya usafiri uko speed miaka inavyosonga, uwezi funga kisa hakuna soko.

2)Managable, usimamizi ni ndogo sana unahitajika na hakuna mahesabu mengi.

3)Risk, biashara ina Assert zinazoeleweka alishindwa biashara unaiwezo wa kuuza na kurudisha pesa chapu.

Fanya uwekezaji mkubwa sana kulingana na ratio za Mtaji wa biashara husika, Design, Muonekano, Location...hata ukiwa unapata faida ndogo kwasasa miaka inavyozidi kwenda gari zinaongezeka soko lake lakueleweka.


Daladala & Bodaboda unamuda kadhaa wa kuchekelea na muda mwingi wa kulia baadae.

Kama huna muda wa kufatilia najiri mimi kutafuta Location, wataalamu wa ku-design mpaka inaanza kazi | utanilipa.

October mana wewe ni mpambanaji sana Heshima yako mkuu
 
Kila mtu anakimbilia biashara ya kuku
Wacha uingie uone changamoto zake
Hii kauri sio Valid kwenye huu ulimwengu wa sasa hakuna Biashara ambayo akimbilii kilamtu karne hii.

1)kila mtu anakimbilia biashara ya bodaboda √
2)kila mtu anakimbilia biashara y uwakala √
3)kilamtu anakimbilia biashara ya bajaji √
4)kilamtu anakimbilia kulima √

Kwa kauri hiyo utatafuta Biashaara ambayo watu wengi wajaikimbia huipati na hutafanya biashara.
 
Dah! Basi tu yani. Kwa kuwa huna uzoefu na biashara ila unatamani kuingia kwenye daladala mimi ngoja nikushauri ila utaamua mwenyewe.

Badala ya daladala agiza IST zako za tu Japan ambapo utatumia kama mil 35 hivi halafu zifanye kazi ya uber ambapo utazikatia na bima kubwa jumlisha ma GPS. Hesabu yake ipo hivi.

Kwa wiki huwa malengo ni 200000 so kwa gari tatu itakua 600 ambapo kwa mwezi itakua unafunga 2m. Hiyo nadhani sio haba kwani usimamizi sio mkubwa pia gari inakua kwenye hali nzuri katika upande wa makenika hivyo mwaka wa kwanza itakua ni nafuu zaid kiuendeshaji wa bashara. Risk zipo kiasi.
Wewe ni jiran kabisa, ukipata nafasi pita hapa ANDO unisalimie
 
Sio uchawi, lakini naona ukienda kuanguka.
Mmechukua mkopo bila kuwa na plan.
Halafu ni risk sana kuanzisha biashara kwa kuutegemea mkopo 100℅

Mna uzoefu na biashara gani?
Kwa usalama wa hiyo pesa kama una kiwanja ni heri ujengee nyumba upangishe.

Neno langu si sheria. Zaidi labda wataalamu waje
Kabisaaa labda akajenge vi apartment apangishe bas
 
NAANDIKA KWA HERUFI KUBWA, USIJARIBU KUFANYA HATA JAMBO MOJA KATIKA HIZO IDEA ZAKO KAMA WEWE MWENYEWE HUTAWEZA KUSIMAMIA HIZO BIASHARA MUDA WOTE (SIO NDUGU YAKO AU WA MKE WAKO).

Kwa nature ya kazi yako, unahitaji kitu ambacho kitahitaji less daily operational activities, mfano ni kama nyumba ya kupangisha

Sent using Jamii Forums mobile app
100% sure!
 
Hiyo ndio sehemu pekee naona hela yake itabaki salama.
AF anasema eti hatoweza kumaliza kujenga! Yaani milioni 45 ushindwe kujenga kibanda cha uwani ukapangisha! AF unachuaje mihela yote ikiwa hauna plan yoyote!
Nawaonea huruma ye na mkewe maskini weeee!!! Mungu awasimamie LA cvyo!
 
AF anasema eti hatoweza kumaliza kujenga! Yaani milioni 45 ushindwe kujenga kibanda cha uwani ukapangisha! AF unachuaje mihela yote ikiwa hauna plan yoyote!
Nawaonea huruma ye na mkewe maskini weeee!!! Mungu awasimamie LA cvyo!
Watu wengine wana bahati baasi mil45 hujajipanga unaifanyia nini. Wamechukua tu.
 
Wazo langu kubwa ni kuagiza gari ya biashara maana sina mda kabisa wa kufanya biashara nyingine maana kazini tukiingia asubuhi kutoka ni jioni kwahiyo nimejaribu kuangalia kama naweza kupata kidogo kitu cha kusogezea maisha yangu maana mshahara siku zote hautoshi ndugu je wew kwa kazi yangu ungenishauri nifanye kitu gani bila kuathiri utaratibu wa kazi .Maana naogopa biashara nyingine naona kuangukia pua kutokana na kukosa mda wa kusimamia
Biashara ya daladala ni kichaa itakufilisi na utajuta hafu unachukuaje hela nyingi huna plan,naona ukifeli na kujuta
 
Back
Top Bottom