DeepPond
JF-Expert Member
- Nov 18, 2017
- 41,728
- 103,997
Mtu hajawahi kufanya biashara,@kisumapai
Nimesoma kwa utulivu ulichokiandika na nimeona haya
1. Katika siku 30, Mshahara wako na mwenza wako unatosha kwa siku kadhaa (tarehe 14 huwa hamna fedha za kutosha).
2. Hamna uzoefu wa biashara.
3. Umesha shauriana na mwenza wako aina za biashara.
Kwa mtazamo wangu fedha igawanye katika namna hii;
1. Biashara A. Hii iwe biashara ambayo itakupatia pesa ya kusaidia kuwezesha matumizi ya familia yako ya kila siku. Hii biashara iwe na uwezo wa kuingiza pesa ambayo ukiichukua haiwezi kuathiri biashara yenyewe.
2. Biashara B. Hii iwe biashara inayoingiza pesa itakayokuwa inahifadhiwa kama kukuza mtaji wenu wa biashara. Hii biashara iwe na uwezo wa kuingiza pesa kwa mwezi angalau faida ya asilimia 30% ya mtaji ulio wekewa (baada ya kutoa garama zote).
3. Biashara C. Hii iwe biashara ambayo itaweza kuingiza faida ya angalau 50% ya mtaji kwa kipindi cha kuanzia miezi mitano hadi nane au mwaka na iwe biashara ambayo unaweza kurudisha faida uliopata na kuongeza kama mtaji na kuipanua biashara hiyo.
Sasa aina gani ya biashara itakua ni biashara A, B na C inategemeana na vitu hivi;
1. Eneo unaloishi au utakalo amua kufanyia biashara
2. Muda utakao kuwa katika usimamizi na uangalizi wa biashara
3. Ujuzi juu ya usimamizi wa biashara ama kuwepo mtu wa kuweza kuangalia taarifa za biashara yako na kuweza kujua mwelekeo wake na kuweza kukushauri nini cha kufanya (iwapo mwelekeo hasi unatokea)
4. Utayari wa kupoteza mtaji (aidha kiasi ama wote).
Biashara inamengi huwezi kuwekeza leo kesho upate faida zingatia hilo na pili kuna tofauti ya mauzo (au pato kutoka kwenye biashara) na faida ya biashara.
afu ndo aanze na utitiri wa biashara.
Tena Ela yenyewe ya mkopo.
Duh! Wallahi mtaita ambyulensi presha itakapopanda
Sent using Jamii Forums mobile app