POLE SANA, Nakuomba sana hiyo pesa irudishe bank au kwa hao waliokukopesha haraka, Pesa ngeni, kazi ngeni , wewe mgeni kwa hakika hiyo ni BALAA, Pesa bila PLAN ni balaa..
Sio kila pesa ni neema inategemea umeipataje na uzoefu nayo na uzoefu wa kazi yake pia n.k,,,
Mimi ni mjasriamali pia tena mzoefu kiasi changu, kwa miaka hii ya karibuni tena kwa shughuli za kuchanganya mikono ya watu au kutumia watu, HAKIKA HAKUNA BIASHARA YA MKOPO 100% ITAKULIPA tegemea maumivu na hasara kubwa BORA UZIRUDISHE HIZO PESA.
Bank au mikopo mingi Riba ni kuanzia 18% na kuendelea na biashara nyingi zinazolipa sana
zinazosifiwa huishia 8% hadi 13% kwa mwaka baada ya kuondoa gharama zote, fatilia
sasa wewe ukodi pesa kwa 20% mfano na zikuzalishie 12% UTAPONA ? ?
Aidha uwe tayari kujifunza biashara/ujasriamali kabla ya kustaafu kwa KUZIPOTEZA HIZO 45 mln na zinaweza kuisha na usielewe chochote ukaambulia kuchanganyikiwa - BAHATISHA
Nikiwa mjasriamali ni DHAMBI SANA KUMKATISHA TAMAA Mjasriamali anayeanza.
Ushauri wangu anza kidogo kidogo bila mkopo au 30/70 mtaji yaani mkopo 30% isizidi kwa mtaji mali yako iwe 70% ukijiwekea malengo makubwa hata kama utaanzia Sh 5mln tu huko 45 mln utafika tena salama na ari nzr na zaidi,
Washauri wamejaa kila aina ya biashara kwa mitazamo yao TATIZO hawana takwimu linganishi za kukusaidia kuamua badala yake sawa na chukua 45mln ukacheze kamali..