Nina Milioni 45, msaada wanaJF

Ushauri wako mzuri Tena akienda nje ya mkoa Kuna maeneo ka kibaigwa huko watu Wana magala na wanalipia kuweka mahindi kwa ushuru
 
Good advice
 
Achana kabisa na daladala zitakufilisi njoo Pwani kuna sehemu uhitaji wa nyumba za kupanga uko juu sana
Kiwanja 20 kwa 20 4M
Jenga vyumba 10 kwa mtindo wa madarasa
Kila chumba ni elfu 30
Kila mwezi una hakika ya laki 3 isiyo na makato
Ngarama ya ujenzi haizidi 25M

Jr[emoji769]
 
Hii sawa kabisa

Jr[emoji769]
 
Duh, pole!
I did the same mistake nilipokuwa nacjukua mkopo wangu wa kwanza, sitasahau miaka ile mi4 ya kupoteza pesa na kuendelee kupokea nusu mshahara. yaani ilokuwa miaka migumu sana ktk maisha yangu.
 
Milioni 45 ushindwe kujenga na kumaliza?

Unaweza nunua hata pagala kuna mapagala unanunua 20 unatumia million 10 kumalizia..

Naona wewe ulivyojenga mwanzo ulipigwa Sana na mafundi..
Hivi mkuu, eti ni kweli kujenga nyumba ukiwa unajua gharama na ufatiliaji pia unajenga kwa pesa nafuu? Hua naskia tu wakisema kujenga sio mchezo
 
Ulipataje iyo pesa bila kujua matumizi. Kama ni ya urithi itaisha bila kujua
 
Kabisa Bagamoyo panafaa kujenga tena mitaa uliko mradi wa malaria sababu viwanja vimeshapimwa na ni sqm 1 tsh 12,000(max) ,ukiingia kichwa kichwa mitaa isiyopimwa umepigwa.

Kujenga andaa m25,jenga nyumba pangisha nzima iwe na fensi ni tsh 250,000 kwa mwezi
 
Kulingana namazingira yako yakaz naupeo wako wabiashara hii ndo biashara sahihi ambayo haitakutesa ninaiamin asilimia 100% kama sio mpunga nunua mahindi weka stoo hiyo pesa kama isipojidouble itaongezeka zaidi ya asilimia Sabin, nalogic ni ndogo tu saiv mahind bado yan 7000.

Nunua mifuko yakinga njaa yakuhifadhia yasibunguliwe kwa bei yajumla inauzwa 4000 @ inabeba debe sita ko pigia umenunua kwa 10000jumla ukusanyaji nausafir mwez kuanzia wakumi mahind debe co chini ya 15 (minimum) hyo ni faida 50% nabila stress kama unavyotaka ukichanganya nampunga hapo faida kotekote. Mimi nimtumishi pia hii business imeniweka mjin trust utakuja shukuru baadae
 
Kwa nadharia uko sawa lakini practically ni tofauti sana naweza sema kwa sasa bora taxi ya kawaida kuliko uber
 
Hujui bei ya Tata ni zaidi ya 100mil?
Hujui kwa mwezi atapata 2.4mil kama atafanya siku 30 ambacho hakiwezekani?
Hapo hujatoa service
Hujatoa emergencies

Kwa mwezi akabakisha sana ni 1mil je atalipia vipi hizo hela zilizobakia kununua gari
 

Sijakataa bali nimempa angalizo kukimbilia biashara iliyopo pasipo ubunifu ni 0 yani mtu unakua wakala haufanyi ubunifu ata wa ofisi?

Sasa wacha wakimbilie iyo biashara ya kuku wataona mziki wake sokoni wateja walewale wauzaji wengi wa kuku, chakula kinauzwa gari n ukizingua bei wanunuzi uwaoni kbxa na kuku muda wa kutok umefik wanakul tu chakula ambapo ni hasara, kutan n chngamoto ya magonjwa kuku wanakua mpk siku 1 watoke wanakufa karibia nusu banda.

Hii business nimeifanya miaka 4 naijua in and out sio namtisha mtu ila inabidi uwe na capita haswa unaweza pata faida mara tano ukaanza na kuku 200 ukafika kuku 1000 ukapata majanga kama ulikua hauna Contigency plan utajuta alafu kumbuka hii biashara imeingiliwa na Macelebrite kama Nandy, Mc pilipili kutake over market inabid uwe smart so kama mtu hajafanya reserch ya kutosha kupata masoko mapya atajuta sana
 
Milioni 45 ushindwe kujenga na kumaliza?

Unaweza nunua hata pagala kuna mapagala unanunua 20 unatumia million 10 kumalizia..

Naona wewe ulivyojenga mwanzo ulipigwa Sana na mafundi..
Huwa nachukia idea ya kununua nyumba iliyojengwa, kwanini usianze yako na ramani yako jinsi unavyopenda,
 
Nani ana michoro mizuri ya banda la kuku lenye usalama wezi wasiweze kuiba na lenye mipangilio mizuri
 
Kwa pesa yako hiyo inabidi kuwa makini sana mkuu kwani hizi hela za mikopo asilimia 95 watu wanazipiga blanda alafu inabaki majuto kwenye makato.
Cha kufanya kwanza usimwage hela yote kwenye biashara moja.

Mimi nakushauri kwa sababu una mtaji mrefu chukua hata m30 au 25 hv wekeza kwenye e-money business na hakikisha unampata kijana mzoefu kabisa na maslahi utampa mazuri kulingana na mwenendo wa biashara.Hapa uchaguzi wa location ndio mchawi mwenyewe ukipata sehemu nzuri then weka M pesa,tigo pesa,aitel money halopesa nmb,crdb,equity kiujumla wakala wa benki zote.

Hakuna muamala utakupita hapa na uzuri wa biashara hii kila siku mtaji wako uko pale pale.Hapa tu zingatia eneo lenye liquidity kubwa na kijana mzoefu plus ofisi iwe rahisi kuonekana.

Kiasi kinachobaki hicho angalia hata kununua longterm asset kama kiwanja na vinginevyo.
 
Madalali wamekaba kila sehemu kuleta ugumu tu ..mbavu zao 😡
 
Umemueleza vyema sana muomba ushauri, hakuna biashara isiyo na changamoto hapa duniani,

Mtoa mada fuata ushauri wa huyu mwamba hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…