Kama kweli umeamua kuingia kwenye biashara Watu wametoa mawazo mengi mazuri sana tu...yafanyie Kazi ondoa uoga kabisa.
Zaidi sana huu ni msimu wa mavuno ,mpunga,mahindi,maharange n.k..,binafis nakuomba ufanye biashara ya mpunga ndani ya miezi mitano hii,yaan sita hadi wa 11 utaweza Ku pata faida nusu au zaidi ya mtaji wako.(sio uanze na pesa zote hizo).. Anza hata na million 10 tu,zingine wekeza tena kwenye biashara zingine.
Biashara ya mpunga au mchele kwa miezi hii ,kuna uwezekano mzuri sana wa kupata faida,ingia porini nunua mpunga kwa bei rahisi nenda kakoboe mashineni uza mchele..zama tena porini.
Kama unaweza zaidi tunaweza kusaidiana kwa makubaliano ya kisheria tukafanya pamoja hiyo biashara kwa sababu nina ujuzi na uzoefu wa kutosha.
Tuwasiliane na pia angalia ushauri wangu na mawazo yangu ambayo nilishawahi kuandika humu...uone labda tunaweza kufanya kitu kwa pamoja.
Asante.