Hauko serious ndugu, eka mia5 kwa mtaji wa 45m?!! Mara ujenge frem ufungue hardware kwahiyohiyo 45m? Yaani ununue kiwanja, ujenge frem (na godown/stoo) then bado ubaki na mtaji wa hardware?!!
Biashara ndugu zinaendana na uzoefu, interest, na kiwango chako cha subira. Nahisi unapenda sana biashara ya magari, kama vipi fanya research upande huo uwekeze huko, huenda nafsi yako itakuwa na amani. Humu kila mtu ataponda kitu hata asichowahi kukifanya au alichokifanya akafeli, kisa tu alifeli yeye au nduguye basi ashaiona haifai, anashindwa kujua kwamba haimfai yeye inamfaa mwingine.
Biashara ya kilimo kwa wanaoijua wanapata pesa na kila mwaka utawaona wanajenga magodown ya kuhifadhi mazao yao. Salum Sumri alikuwa na fleet kubwa mno ya mabasi lakini ameona nibiashara kichaa ameamua kwenda kulima, kama hili halikufikirishi basi hakuna kitachokufikirisha.
Mtihani mgumu kabisa ulionao nduguyangu ni KUANZISHA BIASHARA, hapo ndiyo pesa hufa, na usipokuwa makini kweli hiyo pesa itakufa. Angalia sana ushauri wa humu ndani, wengi humu ni waajiriwa wasio na uzoefu wowote na biashara zaidi ya uzoefu wa kwenye keyboard na failed attempt zao katika biashara waliweka watu wengine wasimamie sababu wanabanwa na kazi. Wengine ni wanafunzi tu ambao hata kuuza karanga hawajawahi.
Kama hiyo pesa unategemea mkopo nakushauri usichukue kwanza, anza na yakwako ikuze taratibu.
Sent using
Jamii Forums mobile app