Nina milioni 8 nifanye kipi kati ya kununua bajaji au kununua gari kwa ajili ya Uber na Bolt?

Kuna muuni pale sinza Mori anauza chipsi mishikaki. Ana nyomi la watu. Biashara ya chips nzuri Sana kama ukiotea sehemu nzuri iliyochangamka hapa town na pia ukapata mtaalam mzuri wa kuzipika na kuandaa mishikaki vizuri.
 
Mkuu endelea na hiyo shughuli yako iliyokufanya upate hiyo pesa mkuu
 
Broh hela zitapotea kiutani utani, tafuta taarifa za kutosha kuhusu kitu unachotaka kufanya. Pia usiwe na au kichwani. Chagua kitu kimoja na uwe na sabab za kufanya hicho kitu.
 
Kama unaendesha mwenyewe chukua gari ufanye uber huku unaendelea na shughuli yako iliyokuwa inakuingizia kipato.
 
Mkuu ungesema uko mkoa gani me nifundi wa simu na nishawahi kumiliki kiduka cha spare nikajakuibiwa,
 
Una experience na mojawapo wa vitu ulivyotaja? Kama ndio basi fanya hicho ambacho una experience nacho. Kama ulishawahi kuwa fundi wa pikipiki basi endelea na hilo la spea. Kama ni dereva wa bajaji au gari basi endelea na hicho. Mil 8 si kiwango kikubwa sana hivyo inabidi uendelee kukuza mtaji zaidi.

Pia kama unafanya biashara nyingine ambayo ndio imekuingizia hiyo mil 8 basi unaweza pia kuikuza biashara hiyo zaidi ili uongeze pesa yako.
 
Cjawahi kuwa fundi pia cjawahi kuwa dereva bajaji nliwahi fanya biashara ya electronic kutokana nabusimamizi mbya nikaifunga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…