Nina milioni 8 nifanye kipi kati ya kununua bajaji au kununua gari kwa ajili ya Uber na Bolt?

Hiyo milioni nane umeipataje? umetumia muda gani kuipta hiyo milioni nane? Mi nafikiria ungeendelea kufanya hiyo kitu iliyokuingizia milioni nane, hizo biashara zingne ulizotaja ni pasua kichwa haswa kama utampa mtu. MIMI NAJUTA HAPA NA HIZI PIKIPIKI MBILI SIJUI NIUZE SCRAPERS?
 
Ok poa na vipi kuhusu biashara ya spea ... hasa spea za magari madogo , pikipiki, au hata vifaa vya simu
 
Asante mkuu kwa ushauri mzuri ubarikiwe sana .... vipi kuhusu biashara ya spea za magari madogo au spea kwa ujumla.. nipe mawazo
Yani milioni nane utanunua spear gani? Au utakuwa unauza side mirror na wiper pekee ???

Maana ukigusa vingine unaambiwa kila kimoja Malaki hapo haujakodi fremu na uichomelee watu wasiingie batini, aisee hiyo usiifikirie kabisa hata spear za Boda achana nazo.

Weka vibanda vya chips vinne sehemu zilizochangamka , nunua boda ya kuzungukia na kupeleka mkaa na viazi kwenye vijiwe vyako ukikomaa kwa siku hukosi laki nne kwa vibanda vuote hapo unaweka milioni zako tano tu mtaji tatu weka za Emergency.

Hata siku ukipata pungufu bado hauna hasara kwa mwezi
 
Mkuu 8m achana na hizo biashara kichaa..

Tafuta a single product ambayo inawateja,,, Agiza kutoka nje then weka margin ndogo tu (vunja bei) ili wateja wako wawe wauzaji wa hio bidhaa...

Hii infanya kazi katika kada yoyote ya biashara.... (Acha tamaa, chagua bidhaa moja tu)

Thank me later..
 
Kanunue mahindi Tunduma huko uje uongeze thamani, sambaza madukani.
 
Kwa nini mkuu huletewi hesabu au?
 
Achana na bajaj na gari fungua duka la spare
 
mkuu ushauri wako mzuri Sana. Ila tatizo linakuja kwenye kukaa na hio 8ml aliyonayo jinsi ya kuisave isipungue Mana ukishika hela tu inatabia ya kuzaa matatizo ambayo utajikuta unaanza kuipunguza taratibu.
 
mkuu ushauri wako mzuri Sana. Ila tatizo linakuja kwenye kukaa na hio 8ml aliyonayo jinsi ya kuisave isipungue Mana ukishika hela tu inatabia ya kuzaa matatizo ambayo utajikuta unaanza kuipunguza taratibu.

Haizalishi matatizo bali wewe ndio unaruhusu changamoto ulizo zivumilia usizivumilie kisa sasa huko na pesa.

Unajua mtu huwezi kutoa ushauri pasipo mazingira. Mazingira kwanza ya favour kutambua wapi uwekeze na wapi usiwekeze.
 
Bora Bajaj maana nauli buku itapiga pesa
 
So kila banda apate laki 1 kwa siku sio? Biashara y chips hata uifanye vp haivuki faida ya elf 30 kwa siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…