Kigoma mjini kubwa,unaishi maeneo gani ya mji huo.
Mwanga,Kilimahewa,Katubuka,Ujiji,Mlole,Kasingirima,Rubuga,Ndahiriwe,Kagera,Bangwe,Kantonga,Kibirizi,Mji mwema,Buzebazeba,Mlole,Katwesunzu,Buhanda Businde,Kitongoni,Livingstone nk
Kila sehem ina nafasi na fursa yake.
Kote huko nimevuruga.
Licha ya kwamba vijana wengi wa pale wanatumia Fursa ya kwenda kuchukua mzigo Zambia na kuuza Hapo mjini na wengine kupeleka vijijini au Mikoa ya Jirani kama Mwanza,Shinyanga na Tabora.
Yaani unakuta mtu unaenda Zambia mfano msimu wa Mananasi hapo mkoani ambapo ni mengi sana kutoka Kijiji cha Bitale na vinginevyo,basi unaenda kule na Mananasi unarudi na Ma Apple,Maziwa ya Kopo,nk.
Au unaenda Kongo kuchukua Vitenge Original kama vile Wax,Soso,Dubai na aina nyingine kulingana na soko na kuviuza kwa bei ya Jumla hapo hapo Kigoma,na kama unaweza unavuka navyo hadi Dar na kuuza kwa jumla wala hukai na mzigo.
Pia unaweza kuja Dar ua Zanzibar kununua vitambaa na kwenda kuviuza Kigoma,hasa Kigoma vijijini inalipa sana.
Jingine nionavyomie,biashara ya Tangawizi kama uki study soko inalipa sana pia,maana Kigoma Vijijini ni miongoni mwa eneo hapa Nchini inayoongoza kwa Ulimaji wa Zao hilo,sasa hii ni fursa pia,ila inahitaji study kidogo.
Ushauri wangu ni kwamba,hakuna maisha ya mkato,ni lazima uingie msituni ujitume sana.Milioni 10 sio pesa ya kujifanya na wewe uitwe Bosi.
Maana mie najua vijana wa mkoa huo kwa masifa ndio wenyewe.