Nina milioni tano nataka kuagiza gari Japan

Nina milioni tano nataka kuagiza gari Japan

Kwa milioni tano!?
bro ukikomaa na ml 5 yako kuagiza gari japan litapigwa mnada unaliona maana bandarini kuna kulipia parking mda ukizidi wakati unahaha kutafuta ushuru mil 5+ nyingine.... baki hapahapa kuna mwamba kanunua carina TImanual mil 4.5 kaitengeneza mil 1.5 ipo barabaran ukiona picha utakataa muhimu ukague gari na fundi mzuri ujue matatizo yapoje.
 
Kuna gari inaitwa nissan duet kwenye show room unapata kwa six mil net... Kwa kuagiza inapungua zaidi ya hapo. Usidanganyike. Nenda katika mitandao ya be forwarded au car junction angalia utafanikiwa tu. Usife moyo. Goodluck
Hamna Nissan Duet
 
Hao wanakwambia uwatafute kwa namba zao za simu kuwa nao makini utalizwa.

Kama unataka gari used be forward ni wazuri ingia utakutana na magari mengi yenye bei tofauti,chagua gari kabla hujalipia nenda tra watakufanyia makadirio ndipo utakapoa amua.

Binafsi nilifanya hivyo na ilinichukua mwezi tu nikaipokea gari yangu
Nimeshaagiza magari kwa ajili ya jamaa zangu mara kadhaa.
Huu ndio ushauri sahihi.
 
Kuna gari inaitwa nissan duet kwenye show room unapata kwa six mil net... Kwa kuagiza inapungua zaidi ya hapo. Usidanganyike. Nenda katika mitandao ya be forwarded au car junction angalia utafanikiwa tu. Usife moyo. Goodluck
Morocan, wewe ndio mmemsaidia huyu mwana JF tofauti na wale wenggine wanao mwambia habari za 10M. Najua akifuata ushauri huu atapata gari ya moyo wake kwani huko kwenye mitandao kuna hata ile calculator ya TRA itakayomsaidia kujua ni kiasi gani atalipia kwa gari anayotamani. All the best
 
Nunua tu bodaboda 2 usimamie kwa makini ndipo upate wazo la kuagiza kirikuu Japan
Unadhani kila mtu anafikiria na kuwa na mawazo ya kiuwoga kama yako acha kumkatisha mwenzako kajichanga hapo alipo .... Kashasema anataka gari halafu wewe una mwambia anunue piki piki huu si ndio uchawi sasa mwenzako anataka kuongeza hatua ww unamrdisha nyuma.

Juzi nimepitia befoward nimeona SUZUKI ALITO CF MILION 2.2 TRA KODI NI MILIO 2.4 sasa hapo hajapata gari? Tujitahidi kujikita katika kumjenga mtu sio kumkatisha tamaaa

sent from HUAWEI
 
Back
Top Bottom