Nina mill Tshs milioni 20, naomba ushauri wa mradi wa kufanya

Nina mill Tshs milioni 20, naomba ushauri wa mradi wa kufanya

Sikasyakamo

Member
Joined
Aug 1, 2015
Posts
36
Reaction score
9
Najaribu kuangalia ni mradi gani naweza kuuanzisha kwa kiasi hicho nashindwa. Naombeni ushauri, eneo nilipo kuna umeme, maji na huduma zingine.
 
Kwa mawazo yangu sina uzoefu na mbeya ila huko nahisi..Biashara ya kusafirisha mazao ina lipa sana
Ifanyie utafiti
ILA uanze na mazao yasiyo haribika haraka kama mahindi, mchele< maharage nk
Ndizi, Viazi, Nyanya yana faida kubwa sana ila yanahitaji uzoefu kwani ndani ya siku nne ukikosa soko unaweza kumaliza mtaji
 
Mkuu hebu nitumie ka milioni 10,hapo chap chap niweke kwenye biashara yangu wakati ukiendelea kupewa mawazo na wadau mbalimbali
 
Vijana wengi na watu wazima ni wapenzi wa michezo... Kwangu mimi ningefungua sports hall la kisasa,kubwa,full mafeni,dstv plus azam tv... Biashara ni competition hivyo wote waliozoea kujazana kwenye mabanda ya makuti kucheki mechi ntawabana.Ndani ya sport hall ningeweka frig kubwa niwabane wateja wangu vinywaji hakika uwa vinauzika kwenye mechi.Lakini uwe na hakika hapo ulipo kuna watu wengi na ni wapenzi wa michezo.mill 20 ni kubwa sana katika hilo inayosalia ni kwa futher investment.
 
fungua duka kubwa kat ya hardware,cafe,au spare parts za pkpk na magal used toka japan kwan vnalpa xna town
 
Back
Top Bottom