Nina millioni 1 na laki 3 nifanye biashara gani?

Bayou98

Member
Joined
Sep 28, 2022
Posts
64
Reaction score
88
Habari zenu wakuu,
Mimi ni mwanafunzi wa chuo nipo mwaka wa pili. Nina jambo langu nahitaji nishiriki nanyi humu ndani.

Nina pesa kama Mil 1.3 nahitaj nifanye biashara lakini biashara niliyonayo kichwani ni kununua pikipiki used ili nimpe mtu awe ananiletea pesa naomba ushauri kwenye ilo.

Nawasilisha kwenu wakuu
 
Nenda Kariakoo nunua Mashuka ya laki 5 tu. Anza kuuza, kama utakuwa mbunifu ndani ya wiki mbili au tatu umeyamaliza na faida ni mara mbili yake.
Shuka zinauzwa 13k wewe unauza 25k wakilia sana uza 22k au hata 20k kulingana na eneo.
Pesa yako itakuwa salama zaidi.
 
Ukinunua pikipiki ya kumpa mtu akuletee pesa, utakuja kulia hapa muda si mrefu!!!
 
Anzisha kijiwe cha juisi ya miwa popote kwenye watu wengi. Weka kijana.
Machine ya petrol n 900k
Deri la kuweka juic 40k
Miwa 10k had 20k
Barafu 10k.
Petrol 10k
Kijana 20k
Ndimu na tangawizi 2k
Hesabu jioni n 100k baada ya kutoa matumizi yote.
 
Kwa Sababu ww ni mwanachuo lazima utaitaji msimamzi pindi utaapokua bize na Mambo ya chuo. Hapo tafuta biashara ambayo risk ya kupoteza mtaji ni ndogo hata kama hausimami mwenyewe muda wote. Ila kwa boda sikushauli ujaribu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…