Nina millioni 1 na laki 3 nifanye biashara gani?

Hiyo mambo ya kumpa mtu pikipiki akuletee hela sio Kabisa tena pikipiki yenyewe used.. Aloo utalia kilio cha mbwa koko
 
Majibu yatategemea upo sehemu gani?
Una malengo na hio biashara kwa muda ganii?
Umejjiandaaje ikitokea risk?

Kwasababu hio hela kwa sasa ni kubwa ila ukianza biashara kubwa utaiona ndogo . Kwahio fikiria (Kwa kukusanya mawazo ya wadau) biashara bora ya kuwa nayo ukiaangalia vipengele vitatu pale juu.

Pia watu wanakupinga hio biashara ya pikipiki maana usiangalie faida Moja kwa Moja kumbuka kuna dharura hutokea kama spear imeharibika tenah used 😭usijelia bure bora ungekuwa na mpunga mzito nkimaanisha mfano siwezi kuwa na million 4 yote nkawekeza katika kitu kimoja ni risk sana
 
Fungua kiduka cha kuuza vipombe vikali na virona na energy drinks iwe maeneo ya watu wengi utapiga pesa vizuri sana hizo hazina Mambo ya leseni.


Vinginevyo nikopeshe kwa riba y a 2.5 kwa mwezi.
 
Anzisha kijiwe cha juis ya miwa popote kwenye watu wengi. Weka kijana.
Machine ya petrol n 900k
Deri la kuweka juic 40k
Miwa 10k had 20k
Barafu 10k.
Petrol 10k
Kijana 20k
Ndimu na tangawizi 2k
Hesabu jioni n 100k baada ya kutoa natumuzi yote.
Nawezaje pata machine inayotumia umeme kukamua juice
 
Wazo zuri ila mimi ninamshauri hizo shuka auze bei ya chini ila awe na mzunguko wa fasta. Kama ananunua kwa 13k auze 15k.

Kwa shuka 100 atapata 200k kama faida. Kama ataziuza kwa haraka itakuwa poa. Faida nyingine ya kuuza haraka ni kutengeneza jina kwa watu wengi.
 
Mkuu shuka 100 uuze fasta
 
Nikopeshe 400,000 Kwa riba ya 20% Kwa mwezi mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…