Nina mimba na mtoto ana miezi minne, naomba ushauri wenu nifanyeje?

Nina rafiki yangu ni mjamzito na ana mtoto mdogo wa miezi 6 bado ana mnyonyesha kama kawaida. Lakini anachukua iron pills na pia anakula balance diet. Kama unaona umeanza kulemewa ningekushauri huyo mwanao mwenye miezi minne mwanzishie baby formula.

Na uanze kuchukua iodine + folic acid tables kumtunza mtoto alie tumboni.

Atakae kutukana nayeye hanaheshima. Mimba ni baraka watu wanahangaika juu chini kupata.

Wewe sio wa kwanza ni wanawake wengi Sana wanafanya hivyo siku hizi ajili ya u busy wa maisha .
 
Kutulia na kuzaa ndio mpango, Cha muhimu hudhuria clinic upate ABC ya kumtunza mtoto aliyezaliwa, aliyeko tumboni na wewe mwenyewe. Mmoja mmoja ndio mpango zingatia Uzazi salama
 
Hormone zimekuwa nyingi mwilini kwaiyo maziwa yake sio mazuri inashauriwa kuacha kunyonyesha kwa muda.pia kibongobongo wanashauri hata asilale nae eti, haina shida yoyote akiweza kujibalance na kama ulivomshauri anaitaji madini ya iron ya kutosha
 
Kwa hiyo nimuachishe kumnyonyesha? Maana bado namnyonyesha na sijawahi kumpa chochote tofauti na maziwa yangu
Jitahidi kumtengenezea balanced diet, protein ni muhimu sana katika umri huo kwani ndio anajenga mwili na kinga ya mwili vyakula vya wanga na mboga mboga na matunda, ikiwezekana blend matunda mpe puree au smooth anywe.
 
hormone zimekuwa nyingi mwilini kwaiyo maziwa yake sio mazuri inashauriwa kuacha kunyonyesha kwa muda.pia kibongobongo wanashauri hata asilale nae eti . haina shida yoyote akiweza kujibalance na kama ulivomshauri anaitaji madini ya iron ya kutosha
Mkuu ukiacha kibongo bongo.

Uangalie Ki sayansi maziwa ya mama mwenye mimba hayanamadhara kabisa kwa mtoto mdogo anaenyonya.

We soma medical journal yeyote kuhusu hili . Uzuri mimi nina mfano hai kabisa ya kwamba hili halina shida.

Google search- is breastfeeding while pregnant safe?
 

Pole sana..achisha kumnyonyesha iyo mtoto mara moja..bila ivyo uyo mtoto atadumaa na kudhohofika sana..tafuta njia nyingine ya maziwa ya kopo kwa mtt..pole sana huko ndio kunaitwa kubemenda..mtt mchanga mnamtaftia mdogo wake[emoji23][emoji23]
 
Pole sana..achisha kumnyonyesha iyo mtoto mara moja..bila ivyo uyo mtoto atadumaa na kudhohofika sana..tafuta njia nyingine ya maziwa ya kopo kwa mtt..pole sana huko ndio kunaitwa kubemenda..mtt mchanga mnamtaftia mdogo wake[emoji23][emoji23]
Sikupanga iwe hivyo na wala sikutarajia kupata saivi, ni bahati mbaya tu
 

Kwa mtt mdogo miezi sita ni stage tofauti na kubwa sana ya ukuaji compared na miezi minne..mshauri aache kumnyonyesha maana ata dalili za kudhoofika kwa mtt zishaanza.na ni sababu ya maziwa yashahairibika..
 
Acha kunyonyesha haraka sana bila hvyo utamuaharibu mtt anza kumpa mtt maziwa ya lactogen 1 na akifikisha miez 6 anza kumpa vyakula lain lain
 
Kwa mtt mdogo miezi sita ni stage tofauti na kubwa sana ya ukuaji compared na miezi minne..mshauri aache kumnyonyesha maana ata dalili za kudhoofika kwa mtt zishaanza.na ni sababu ya maziwa yashahairibika..
Na wewe umepata wapi hayo unayoyasema ?
 
nimesema kwa muda mkuu,inashauriwa hivo maana mili una mtifuano wa hormones sasa hivi
 
Lactational amenorrhoea haijasaidia apo
 
Cha msingi wewe endelea kumnyonyesha ikifika miez6 mchanganyie misos mingne
 
Na wewe umepata wapi hayo unayoyasema ?

Me ni mchambuzi wa mambo na nna experience nzuri tu ya kulea..nilivyokua nafanya parenting a nurse alieleza vyote ivyo..nyege zangu zote zilikata maana ni ukweli na ukitaka kuangamiza mtoto fanya ivyo..kama hauna 24,000 za kopo la maziwa kila week unabemenda mtoto..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…