Nampenda sana single mama wangu. Unajua kwanini niliamua kumwoa yeye?
Nilikuwa na machaguo manne. Mmoja alikuwa muuguzi, wa pili na wa tatu walikuwa mabinti wako kwa wazazi wao. Wanakula na kuishi free. Wa nne single mama, anapambana kulea mwanae bila msaada wa baba mtoto.
Yuko kwa wazazi lakini hawamsaidii kumtunza mtoto. Anapiga vibarua na mtoto mgongoni.
Nilimchagua single kwa kuamini kuwa kapigwa na maisha na atakuwa na akili. Na ni kweli ana akili za maisha. Hakuna kumpangiabkazi. Anapanga, anatoa taarifa au kuomba kuwezeshwa kisha anafanya. Na chenji ikibaki nitaonyeshwa au kuelezwa matumizi.
Msichana miaka 19 anajua nini kuhusu maisha? Ni mtoto na kichwani hazimo. Katoka kwa wazazi wake akilelewa kama broiler na kuja kwako. Hajawahi kupigwa na upepo wa maisha.
Mvumilie tu, akiongezeka hadi 25 hivi, akili itapevuka na atakuwa mke mwema.
Kwa sasa kuwa mpole tu kijana wangu. Hawa mabikira wanahitaji kubikiriwa hadi akili.