Nina mpango wakuzuia TV nyumbani kwangu naona watoto wanaharibika

Nina mpango wakuzuia TV nyumbani kwangu naona watoto wanaharibika

Wakuu za usiku.

Nina TV na madishi ya azam na mengine. TV mbili. Nawaza hapa, enzi zetu hatukuwa na TV hivi sasa watoto wanapoteza muda kwenye katuni na movies. Hii inanipa picha najenga kizazi cha kukaa na kuangalia TV, Watu wavivu, Ombaomba na Maskini. Hii haikubaliki

Naomba kutoa hoja..naomba mniunge mkono au kutoa maoni
Wapangie ratiba. Inavyoonekana umewaacha huru sana kwenye TV.
 
Hakikisha wana ratiba ya kufanya kazi za nyumbani bila kujali jinsia, hapo kwenye kazi zingatia muda sana. Hapo uwe mkali kabisa na kwa atakaenung'unika au kuleta ubishi dili nae vilivyo.
 
Wachanganyie na contents unazotaka, waangalie vyote. Mfano unaweza ukadownload kitabu au programu yenye masomo ukaweka kwenye flash disk, muda fulani uwalazimishe waiangalie.
Mimi nimepakua kitabu, nikaweka kwenye flash baada ya kukivonvert kutoka kurasa za pdf kuwa files za picha, waangalie kupitia USB ya TV
 
Mkuu pole sana. Hili la TV kwa watoto ni janga la taifa. Nilishtuka siku moja saa nane usiku nasikia kama watu wanazungumza siting room kwa sauti ya chini sana nikadhani nimevamiwa na majambazi lakini nilichokikuta roho iliniuma sana. Nilikuta TV ipo on sauti imeshushwa sana halafu watoto wamelala nikajua tu walikuwa wanaangalia TV usingizi ukawapitia. Wakati naenda kulala kwenye saa nne hivi niliwaambia zimeni TV mkalale kumbe hawakwenda kulala.

Toka siku hiyo nimekuwa mkali sana. Sasa hivi TV watoto wanaangalia kwa ratiba maalum niliyopngwa tena baada ya kumaliza kazi zao za nyumbani na shuleni. Japo mwanzoni ilikuwa ngumu lakini sasa hivi ratiba inafuatiliwa niwe nipo au sipo au hata kama nimesafiri kwa sababu wanajua wakizingua tu hata ratiba niliyoweka naifuta kama adhabu.
 
Pdf yake ni ndefu kidogo ila kanuni ya malezi ni kwamba watoto hawafanyi kile unawaambia wasifanye au wafanye Bali hufanya kile unachofanya
Wakiume hufanya kama baba yake na WA kike hufanya kama mama yake kuanzia wakati wa kuamka hadi wakati wa kulala
Sikiliza "coward of the county"wa Ken Rogers utaelewa vizuri zaidi ni SoMo la malezi nami sio mzuri sana wa kuandika
Hata You Tube kuna programs nyingi za jinsi watoto wanavyofuata zaidi wanayoyaona kuliko wanayoambiwa, be good most of the time and you children will copy that.
 
kama mtoto wako anaangalia tv sana ujue social life yake haipo vizuri

hana marafiki hapo mtaani, na hachezi michezo kama mpira, baiskeli nk.

1. mfundishe kupenda michezo na kutengeneza marafiki

2. fanya kama wazungu, siku za wiki tv inaangaliwa kwa ratiba... weekend ndo ipo free
 
Mkuu ni kuwawekea tu ratiba maana huwezi kushindana na teknolojia mwisho wa siku itashinda. Hata kabla ya zama zako kulikuwa na zama za wa kabla yako nao hawakuwa na vitu ulivyokuwa navyo wewe huenda na wao walikuwa wanakuona wewe mvivu.
Just wawekee muda tu na ratiba. Teknolojia si mbaya ikitumika ipasavyo. Kwa mfano mimi nina kiajana mtoto wa dadangu ana miaka 10 nishaanza kumfundisha programming. Nishaanza kumfundisha namna ya kutumia Chatbots kuandika vitu, kuuliza maswali, kupata ufafanuzi. Hopeful mpaka anakuja kufika labda form two atakuwa ana uelewa mkubwa na huenda atakuwa tayari ana uwezo wa kuandika viprogamu fulani fulani.
Umefanya jambo lenye maana dunia yote kwa hyo mtu
 
kama mtoto wako anaangalia tv sana ujue social life yake haipo vizuri

hana marafiki hapo mtaani, na hachezi michezo kama mpira, baiskeli nk.

1. mfundishe kupenda michezo na kutengeneza marafiki

2. fanya kama wazungu, siku za wiki tv inaangaliwa kwa ratiba... weekend ndo ipo free
Nimejiuliza nikapata majibu kama yako. Mbona mimi nilikuwa ba nyumbani kuna TV na nilikuwa naachana nayo naenda kucheza? Tatizo watoto wa siku hizi wanashinda ndani tu. Wazazi wanaona ndio 'uzungu' Sasa mtoto muda wote yupo ndani attachable kuwa addicted na TV?
 
Nje huko unakujua mkuu? Ndani ya jiji sio salama kabisa.
 
kama mtoto wako anaangalia tv sana ujue social life yake haipo vizuri

hana marafiki hapo mtaani, na hachezi michezo kama mpira, baiskeli nk.

1. mfundishe kupenda michezo na kutengeneza marafiki

2. fanya kama wazungu, siku za wiki tv inaangaliwa kwa ratiba... weekend ndo ipo free
Ya ile ya girl friend na boys friend kesho anakuambia nina rafiki yangu, kesho tena jumamosi tutaenda kusex kwa mara ya kwanza. Ilimtokea jamaa angu kitaa.

Maana ilianza safari za kuwapeleka bichi, baadae wanaenda bichi na majirani, baadae ameejnga ukaribu na jirani na mara wanapiga romance
 
Kiufupi dunia imefika sehemu ngumu kwa jamii maskini
 
kama mtoto wako anaangalia tv sana ujue social life yake haipo vizuri

hana marafiki hapo mtaani, na hachezi michezo kama mpira, baiskeli nk.

1. mfundishe kupenda michezo na kutengeneza marafiki

2. fanya kama wazungu, siku za wiki tv inaangaliwa kwa ratiba... weekend ndo ipo free
Asilimia kubwa humu mnaongea maigizo.

Malezi hayajatofautiana na zamani. Nilazima mtoto aishi kwa sheria baaas, hakuna kuangalia tv, hakuna kwenda kwa jirani kuangalia, ni kazi za nyumbani kacheze muda huu umerudi kwisha, hata hiyo ruhusa ya michezoni atatafuta mwanya wake, ni kazi za nyumbani maasaa yoote
1. Kulima
2.kusombea maji
3. Kuuza biashara
4. Kufua
5. Kwenda shule na kuwahi kurudi
6 hata kusoma atatafuta mwanya
7. Akifeli mikwara ya kutosha
8. Atatafuta muda na ataupata
9. Kikubwa usimnyanyase
10. Hakuna kitu inaitwa birthday celebrations never
 
Ya ile ya girl friend na boys friend kesho anakuambia nina rafiki yangu, kesho tena jumamosi tutaenda kusex kwa mara ya kwanza. Ilimtokea jamaa angu kitaa.

Maana ilianza safari za kuwapeleka bichi, baadae wanaenda bichi na majirani, baadae ameejnga ukaribu na jirani na mara wanapiga romance
hayo mambo yatafanywa sana tu

unatakiwa uwaelimishe kuhusu madhara ya ngono kwenye umri mdogo
 
Back
Top Bottom