Nina mtaji wa 2M naomba wazo la biashara

Umesahau na kumwambia anunue na mafuta ya kula nayo dili mtaani
 
Ebhana nimependa idea Yako,kama uko Dodoma hebu tuongee hii issue njoo Dm.
 
wazo nzuri mkuu ishu location tu
 
Uza unga wa ugali mwanangu, tafuta mashine ya kusaga na kukoboa, cheki bei ya mahindi sokoni. Uwe na both Sembe na Dona na mzani, angalia wewe utawachangiaje wenye mashine ila wengine hawana noma sababu unalipia huduma za kusaga na kukoboa. Hio biashara might give you a hell huge profit hadi ushangae sema ndo hivyo kama bishoo hautaiweza.

2. Fanya biashara ya Pumba, njoo morogoro vijijini kwenye mashine za unga, nunua pumba gunia hata 10 kwa kuanzia za debe 10 kwa laki 2 na nusu, peleka dar hasa maeneo ya Goba, Bunju, Mbweni, piga maokoto yako. Kama unajiweza unanunua hata na Mashudu ya alizeti unaenda kuuza mjini, ni biashara nzuri sana na ina faida kubwa sana.
 
Shukrani mkuu
 
Hizo pumba na shudu ni kufika na kuuza tu chapu au ndo mpka uanze udalali
 
Kwan hizi pumba zinatumika kufanyia nini??
 
Ukitaka kufanya biashara yoyote ile ni vyema uijue vizuri kabla ya kuifanya.

Nakushauri kama nguvu unazo, tafuta boda boda, kaa kijiweni au sajili bolt uanze kazi, faida utakayopata unaweza wekeza sehemu nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…