Nina mtaji wa milioni kumi; nifanye biashara ipi kati ya hizi nilizochagua?

Hapo nmekupata japo kuna sehemu Dar hyo business ya vyombo vya ndani inafanywa na watu wengi kwny hilo eneo lakn wote wana mzunguko mzuri
 
Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu amfanyaye mwanadamu kuwa Kinga yakee....ushawahi jiuliza uyo mganga akifa utafanyaje...mganga mwenyew anategemea pumzi ya Mungu Mkuu kuishi
Huku kusini kulikuwa na daktari mmoja akiitwa mwambe huyu ndie alikuwa daktari bingwa wa mifupa kusini yote hii ilimtegemea yeye ila alipofariki wakatokea wengine na wanasaidia watu
 
mwanzo hii sikuwahi kujua siri iliyo ndani mwake mpaka nilipoalikwa kwenye sherehe kama mbili hivi za daycare kama mgeni rasmi ndo nikajua tena baada ya kumkuta professor akaniambia na yeye anayo shule ya hivyo.
 
kwangu mimi ningekushauri ufanye biashara ya kwanza kwa haraka ndio naona nafsi yako inaitazama kwanza na ndio maana ni ya kwanza hata kuitaja.
biashara hii haihitaji mtaji mkubwa sana na hasa ukiuza vyombo vya watu wa kati na mama lishe hivyo mtaji wa m6 unaweza tosha kwa kuanzia.
katika vyombo vyako weka vyombo vya kawaida vingi na vile vya thamani vichache 70:30 itakaa sawa.
 
Mkuu twende No.3 nina aunt yangu alimpandia mtu kariakoo pale mpaka kumtoa mil28 na kodi analipa 600k kwa mwezi.

Japo umetuwekea limit ila kuna biashara ya spare hii mkuu ukipata watu sahihi kutoboa ni 90%.
 
kitaaluma na kadri ya vimafunzo vyetu tulivyofundishwa vingine kwa kugoogle na vingine darasani unaweza kufanya yafuatayo kabla hujaamua kuchangua mradi:-
  1. uwezo muda na uzoefu wa biashara unayotaka kufanya
  2. kuna faida?
  3. soko likoje? hapa tunazungumza uhitaji na idadi ya wauzaji wengine?
  4. mtaji
  5. uchangiaji wa mahitaji ya familia ukoje?
 
Hapo nmekupata mkuu nahsi kwny uthamani wa vyombo itategemea zaidi na location ntayoipata na aina ya watu wanaopatikana hapo...
 
Hakika hvi ni vitu muhmu sana ubongo inabdi utulie sana hapo
 
Ndioa maana vibiashara vyenu havidumu.. mnakuja kulia lia humu.

Kila kitu lazima ukifanyie tathmini na sio kwenda blindly..

Proposal na Biz plan ni muhimu. Hayo uliyoyataja maswala ya kutafuta taarif field, kwa waliotangulia etc ni moja ya feature za biz plan.

Pre assessment kwanza na sio ujitumbukize humo then uanze kulaumu watu labda kama hela sio yako, ila hela hizi za mikopo au za kukusanya muda mrefu kwa jasho na damu unatakiwa uende kwa umakini mno mno.
 
Anachotakiwa ni kuwa na connection na warehouses, ikitokea mtu kataka mifuko mingi kwa muda mdogo anavuta waya mifuko inakuja kwa haraka.

Cement, nondo, mbao, mabomba sio vitu vya kuumiza kichwa.

Hapo akili awekeze ktk vifaa vya Umeme aweke mzigo unaoeleweka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…