Nina mtaji wa milioni kumi; nifanye biashara ipi kati ya hizi nilizochagua?

Nina mtaji wa milioni kumi; nifanye biashara ipi kati ya hizi nilizochagua?

Huo ndio ukweli biashara inaendena na waganga mimi nakuambia hivyo kwa uzoefu nimezaliwa katika familia ya wafanyabiashara na mimi nafanya biashara
Ni uongo. Au niseme ni imani potofu. Kama unasema ukweli basi nakuhakikishia kuwa huyo mganga mnayempa fedha anakula fedha bila jasho. Biashara yenu mnaweza kuifanya hata hizo dawa. Mna kipaji cha biashara lkn hamjiamini.
 
Mkuu achana nae huyo hajui mambo ya biashara ground yalivyo. Huyo ye ana uhakika mwisho wa mwezi anapokea take home yake bila shida. Biashara haijui kabisa, we andika namba hapa nikutwangie unipe muongozo.
Unaongea kitu usichokijua
 
Vipi hao waganga nao ni matajiri/wana mafanikio?
Au ndiyo mganga anaishi kwenye kijumba cha udongo halafu unamfuata akupe dawa ya biashara.
Siyo mfanya biashara kwa sasa ijapo niliwahi kufanya biashara miaka ya 2006-8 huko.
Nilichokigundua ni vigumu sana kulinda biashara yako isiharibiwe na walimwengu.

Kazi ngumu kwenye utafutaji wa fedha siyo kuitafuta bali ni kuilinda na kuitunza.
 
Naunga mkono hoja hata mimi biashara yangu ya majeneza kuna kipindi iligoma kabisa mpaka nikawaza nifunge tu nirudie kazi yangu ya zamani (wizi wa mafuta ya transformers)
Lakini kuna mganga nilimpata kipindi hicho alikuwaga ameletwa hapa Dom na kigogo mmoja wa serikali nikatonywa na chawa mmoja wa kigogo huyo nikamtafuta huyo mtaalam tukaelewana akaja kufanya setting hapa ofisini yaani biashara ilikubali mpaka nikaona sasa naelekea kuwa bilionea!
Baadae hali ile ilipungua tena nahisi nilitakiwa kurenew setting ila tatizo nilipotezaga namba za yule mganga halafu yule kigogo naye alishahama hayupo huku ila natamani sana ningepata tena mganga kama yule ningekuwa mbali
Hapo ni corona ilikuokoa kwa kusababisha vifo vingi we ukahisi ni kazi nzuri ya mganga.
 
Naongea kitu nachokijua. Hakuna dawa, hakuna uchawi kwenye biashara. Ni imani yako tu. Unaweza kupewa hiziri, ukajiamini kwenda kufanya biashara na ukafanikiwa. Kungekuwa na uchawi hakuna mtu angekuwa maskini.
Mbona Mashamba yapo na misitu pia yenye rutuba ila watu wanashindia njaa?
 
Wee
Naunga mkono hoja hata mimi biashara yangu ya majeneza kuna kipindi iligoma kabisa mpaka nikawaza nifunge tu nirudie kazi yangu ya zamani (wizi wa mafuta ya transformers)
Lakini kuna mganga nilimpata kipindi hicho alikuwaga ameletwa hapa Dom na kigogo mmoja wa serikali nikatonywa na chawa mmoja wa kigogo huyo nikamtafuta huyo mtaalam tukaelewana akaja kufanya setting hapa ofisini yaani biashara ilikubali mpaka nikaona sasa naelekea kuwa bilionea!
Baadae hali ile ilipungua tena nahisi nilitakiwa kurenew setting ila tatizo nilipotezaga namba za yule mganga halafu yule kigogo naye alishahama hayupo huku ila natamani sana ningepata tena mganga kama yule ningekuwa mbali
Wee jamaa 🤣🤣🤣🤣
 
Mbona Mashamba yapo na misitu pia yenye rutuba ila watu wanashindia njaa?
Kwa sababu ili shamba au msitu ukiletee chakula kuna kufanya kazi kubwa sana inayohitaji muda, mtaji na wakati mwingine unaweza kupata balaa usifanikiwe. Uchawi kwenye biashara siyo hivyo na pengine wewe ni tapeli unayenyemelea watu ajinga uwapige hapa JF.
 
Dogo unafeli mimi siwezi kumtapeli mtu na hapa nipo wazi mimi naitwa Mnachihangu kwa wakazi wa mtwara mjini kwa maeneo ya sokoni hakuna asienijua
 
Dogo unafeli mimi siwezi kumtapeli mtu na hapa nipo wazi mimi naitwa Mnachihangu kwa wakazi wa mtwara mjini kwa maeneo ya sokoni hakuna asienijua
Kwani kujulikana ndiyo kunazuia mtu asitapeli? Tena kwenye haya mambo ya uganga ndiyo rahisi kweli kweli kwani huwa hakuna kipimo. BTW kama uko huko Mtwara nitakusamehe kwani sehemu nyingine imani za uchawi ni kama utamaduni.
 
Hapo ni corona ilikuokoa kwa kusababisha vifo vingi we ukahisi ni kazi nzuri ya mganga.
Hapana mkuu kipindi cha Corona ndo biashara ilinigomea sana mpaka nikahisi kuchanganyikiwa niliwekeza kama 7m halafu za mkopo nikawa naamini kwamba watu wengi wangekufa ila cha ajabu mambo yakageuka misiba hakuna na akifa mtu eneo hilo ni muislamu duh!
Ila kipindi ambacho nilipata mganga ilikuwa corona ishapita
 
Hakuna mganga anayeweza kukupa dawa ya biashara,yeye na familia yake masikini halafu akupe dawa ya biashara!kama anayo si angewapa watoto wake au ndugu zake.
Mnajiongopea tu,ingekuwa hivyo Afrika ingeongoza kwa kuwa na matajiri wengi Duniani.
Ni sawa na kusema hakuna muuza samadi ambae yy masikini anaeweza fanya shamba lako listawi kumzidi maisha
 
Back
Top Bottom