Nina mtaji wa sh million 6 ambayo mpaka sasa sijajua exactly ni biashara gani nifanye

Nina mtaji wa sh million 6 ambayo mpaka sasa sijajua exactly ni biashara gani nifanye

Katika biashara ambayo Inahitaji usimamizi na uwepo wa karibu basi ni hiyo miamala..
Asidanganyike akatia hela zote huko, uaminifu kwenye pesa ni mdogo hata ukipata mwaminifu bado kuna changamoto ya matapeli!
Ni kweli mkuu mtu unayemwachia akifanya uzembe kidogo tu anapoteza laki 5 kwa mara moja.
 
Habari ya muda huu wakuu.
Mimi ni msichana wa miaka 24, nimeajiriwa katika kampuni ambayo masaa 8 nakuwa kazini na ninaishi dar-es-salaam nina mtaji wa sh million 6 ambayo mpaka sasa sijajua exactly ni biashara gani nifanye ili kuizalisha pesa hiyo na bila kuingilia ratiba yangu ya kazini maana nafahamu biashara nyingi zinahitaji usimamizi wa karibu sana ili kuepusha vitu kama kutapeliwa pesa.
Nilishawahi kufanya biashara ndogo ndogo nikiwa chuo kama kuuza nguo na viatu kwa wanachuo wenzangu wa jinsia ya kike.
Kwa kuileta mada hii kwenu nina imani nitapata msaada mzuri wa mawazo ya biashara kutokana na hali yangu halisi ilivyo.
Ahsanteni.
Buy bitcoin.
 
Fanya online forex Trading, mtaji wa kutosha kabisa huo, tunza pesa yako jifunze kwanza and you will thank me later
 
Back
Top Bottom