Nina mtaji wa Tsh. 200 Milioni, ninataka kuwekeza katika biashara ya mbao kule Mafinga

Nina mtaji wa Tsh. 200 Milioni, ninataka kuwekeza katika biashara ya mbao kule Mafinga

Ma learner uta wajua tu hayo masaa yako kwa mwendo wa tractor hapo sawa. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji117]
Tuliza wenge! Natumia Mitsubishi double cabin L 200 Spotero!! Nikijivuruga sana Makambako Mbeya ni 1 and half hours,pale ni 182kms!! Sasa Mbeya mafinga unajua ni kms ngapi? I doubt ni sehemu ambazo huzijui au unapitaga tu
 
Mkuu ninayo chain saw ntakukodishia ikusaidie kwa kazi zako ukiwa tayari unichek
 
200000000 dah aisee siku nikizipata hizi kwanza nanunua gari ambalo juu liko wazi.pili nanunua nyumba tatu naweka fixed account nabaki na million 20 tu za biashara ya kunipa wese route za singida dodoma dar masasi songea mtwara ...ni full unyama
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] unatafuta na pisi kaliiiii usahau shida kwa mda kidogo
 
Biashara ya mbao itakulipa sana mkuu , Nina uzoefu mkubwa wa biashara hiyo ,na ni biashara ambayo inaendesha maisha kiujumla
 
Hakuna mfanyabiashara hapa. Pia wewe sio Mkenya ingawa umejitahidi uonekane hivyo. Uzi wako umeibua maswali mengi.
 
Habari Wana JF,

Mimi ni mwanabiashara kutoka Nairobi, Kenya. Ninafanya biashara katika sekta za Ujenzi na Real Estate.

Katika pilka pilka za kibiashara, nimekuja kuugundua mji wa Mafinga. Mji wa Mafinga unajulikana kama mji wenye mbao na miti mingi zaidi Tanzania. Kwa sekta yangu ya Ujenzi hapa kenya, kuna demand kubwa sana ya Mbao kwa hivyo soko itakuwa ni hapa Kenya.

Kama nilivyosema kwenye mada, nina mtaji wa millioni mia mbili pesa za Tanzania.

Ningependa kuwekeza katika hii sekta ya mbao kwa kuweka sawmill hapo mafinga.

Je, ni kweli kwamba miti iko available easily?

Biashara hii wakenya tunaruhusiwa kujihusisha nayo pia?

Ninaweza kupata shamba la ku-lease ili niweke hiki kiwanda? Kulease kiwanda itagharimu pesa ngapi hivi per acre.

Mapato ya hii sekta hukuwa vipi?

Bei ya sawmill kule Tanzania ni pesa Ngapi? Hapa Kenya inaanzia Tsh. 60 million kuendelea.

Bei ya miti mafinga ni ngapi hivi?

Nikifanya biashara Mafinga nitaishi wapi? Ningependelea mji ambao ni upper-middle class kwendelea.

Kuna Ndege zinazokwenda route ya Mafinga au Iringa to Arusha?

Kuna taratibu nyingine maalamu kwenye hii biashara ambazo ninafaa kuzijua?

Je, hii biashara inalipa?

Ninaomba ushauri wenu.

Ninashukuru.
Mkuu, kwenye hiyo pesa yako chukua nusu yaaani 100 millions kisha weka akiba bank alafu nyingine inayobaki ndio jaribu biashara.
 
200000000 dah aisee siku nikizipata hizi kwanza nanunua gari ambalo juu liko wazi.pili nanunua nyumba tatu naweka fixed account nabaki na million 20 tu za biashara ya kunipa wese route za singida dodoma dar masasi songea mtwara ...ni full unyama
Kazi na bata ili kupunguza stress
 
Hela yako ni nzuri kwa hiyo biashara.
Ila napenda kukueleza ukweli kuwa kama wewe sio mzawa wa Tanzania na pia huko mafinga stop that business hutafika mbali .

Usumbufu ni mwingi hasa vibali, bado haujakutana na matapeli na wenye roho za husuda.

But all in all kama unaweza biashara ya kimafia basi hapo ndio pake ingia utapiga hela ila kama ni biashara za kunyooka tu unategemea ufanye huko , ndugu fanya mambo mengine.

Ukiamua kuinvest Tanzania kwenye jambo tofauti na hilo karibu tuelezane safi na chafu.

Cc Mshana Jr
 
Ni kweli mji wa mafinga, na mufindi yote kwa ujimla pia mkoa wa njombe kuna miti mingi sana mbao nyingi sana za kutosha.

Kuhusu makazi pindi utakapo kua Tanzania kama uta chagua mafinga tafuta nyumba hapo hapo huwezi kukosa, pia mafinga hakuna kiwanja cha ndege hata iringa sidhani labda uchukue ndege ya arusha Dar mbeya ukitua mbeya uchukue costa mpaka mafinga sio mbali ni mwendo wa saa moja na nusi au saa moja tu kuhusu kibali cha kusafirisha Kenya sifahamu na menginyo wanakuja.
Mbeya - Mafinga kwa gari binafsi 2½hrs+
 
ukifungua kampuni utakuwa kama muwekezaji, hiyo hela haitatosha. wenzako wanaolima vitunguu mang'ola na himo wanakuwa na watu wao amabao ni wenyeji wa nchi. wanafanya mambo zao kwa kivuli cha watz. niko hapa nikusaidie hatua kwa hatu
 
Kuna fundi ujenzi namjua ni mkazi na mwenyeji wa Iringa kama utajali naweza kukupa mawasiliano yake inbox uenda akakupa dondoo mbili tatu
Fundi ujenzi na biashara za uvunaji miti wapi na wapi. Hii inatakiwa mtu aliewagi kufanya hiyo biashara kutoka huko.
 
Back
Top Bottom