Tafuta zile karanga nene, kazichomeshe vizuri bekari (bakery) usichome kwa mchanga na chungu...hlf funga vifuko vya saizi vya plastic uza kwa jero au mia 3 kila kifuko....hlf tafuta kijiwe chenye njia ambayo watu wanapita na kupituka mara kw mara yaani hawakauki...baada ya mwezi watu kukuzoea utakuja kuleta mrejesho chanya hapa...note, njugu zako usipunje tia kiasi cha kuwavutia wateja walau kwa kipindi cha mwanzo wakt unatambulisha bidhaa yako...na njugu hizi ni plain usitie yai wala kitu chochote.ila hakikisha tu zinachomwa vizuri hlf ziwe zile mbegu nene sio ndogo ndogo.