Nina mtaji wa Tsh Milioni 20, nataka kufanya biashara ya ng'ombe

Nina mtaji wa Tsh Milioni 20, nataka kufanya biashara ya ng'ombe

Ng'ombe wa kupeleka pugu hawezi kununuliwa laki tatu, hata laki nane ni kubahatisha sana.

Cha kwanza ajitahidi kutembelea soko la Pugu kwa minada mfululizo hata kumi. Kisha akatembelee minada ya mikoani atakapokuwa anawatoa hao ng'ombe
Huo ushauri wa kutembelea minada ni muhimu sana
 
Sidhani kama ni sahihi Mkuu, ukienda minadani Ng'ombe mmoja huuzwa kati ya shilingi 300,000-800,000 ambapo kwa hela hiyo hakosi ng'ombe 30 na usafiri hadi Dsm.

Ambapo hakosi faida ya shilingi 2,500,000 ambayo sio hela ndogo usawa huu
Kanitisha sana aisee
 
Nawasalim kwa jina la muungano!! ,

Wakuu nina mtaji wa 20m nataka nianze biashara ya ng’ombe kutoka mikoani nakuleta Pugu DSM, naomba kujua ABC za hii biashara na kama inalipa au lah
Usiingize hela yote kama mtaji sana anzia na 10m ukizidi 15m

Mwisho hakikisha humuamini mtu nenda front mwenyewe
 
Kabla hujaingia kichwa kichwa nenda kafanye utafiti mwenyewe huko Pugu kaa hata wiki uone namna mifugo inavyoingia na kuuzwa

Angalia wakifika, wanafikishwa wapi na wanalipa ngapi kwa kuwapumzisha na chakula pamoja na maji
Je madalali wakoje

Kuna changamoto nyingi sana katika hiyo biashara
Ila ukipambana na kuzijua ABC basi huna shida, ila usiingie kichwa kichwa

Lazima ujue bei zake pia kama zinalipa
 
Back
Top Bottom