Nina mtaji wa Tsh Milioni 20, nataka kufanya biashara ya ng'ombe

Ipi hiyo boss?
 
Nipe ABC ya mbuzi mkuu.
 
Nipe ABC ya mbuzi mkuu.
Uwe na mtaji.
Manunuzi kwa mbuzi wengi ni dodoma minadani.
Uwe na mtu anaeifahamu minada na anafahamika na magalagaja wa minadani.
Manunuzi yanaanza asubuhi mpaka mchana kazi imeisha.
Baada ya manunuzi ataachumiwa mshagaji atapakia kwenye gari kuwaleta mjini kwenye kituo cha uhifadhi.
Gari utalipia,mswagaji na kituo cha utunzaji.
Utazunguka minada kadhaa kukusanya,ukitimiza idadi kulingana na mtaji wako utakodi gari kama unao wachache utaunga gari na wengine ila lazima mbuzi wako uwawekee alama maalumu.
Kituo kikuu cha mauzo ni pugu.
Pia waweza andaa wateja wako.

WAKATI NAFANYA 2018
Mnadani kwa kila mbuzi ushuhuru 2000
Pungu kwa kila mbuzi ushuru 2000
Maji na majani ya kulishia utanunua
Wapakiaji na washushaji utawalipa ww
 
Hakuna biashara rahisi hata kidogo nashangaa kuona watu wengi wakitoka negative sana kwenye hii biashara ila cha kushangaza kila siku ng'ombe zinachinjwa na nyama inalika. Kwani wao wanaofanya sio watu na swali la msingi nikujua jinsi yakupambana na changamoto hizo za biashara full stop. Muomba ushauri anzia pugu pata ABC za biashara then ingia mzigoni usikatishwe tamaa eti kwa sababu flani alifanya akashindwa na ww ukifanya utashindwa hiyo ni BiG NO. Kushindwa kwake ni kushindwa kuhandle changamoto hiyo biashara. Utamu wa ngoma ingia kati ucheze mwenyewe bro. Ukitaka kujua kuwa hakuna biashara rahisi. Andaa uzi mwingine wa hizo biashara ambazo umeambia ni bora ufanye kuliko hiyo ya ng'ombe alafu utaona wadau watakavyokuambia changamoto zake na mwisho watakupa mawazo mengine ya biashara zingine. Nawasilisha
 
Mkku nami naitaji muongoz nimekufata inbox!
 
Hii imetoa mwanga sana sana
 
Msaada nenda Pugu utapata ABC kwa hao wauzaji. Sidhani kama wamo humu.

Siyo kejeli ila ni ukweli.

Ni biashara inalipa kama utavumilia nakushauri kachukue msukuma mmoja anayenunua mikoani uungane naye. Ni waaminifu .
Sahihi
 
Kwa mtaji wako tafuta biashara nyingine labda ingekuwa m200
Mbona mnapenda kukatisha tamaa watu, ml 20 ni ndogo wakati ng'ombe mkubwa ana range 400000-1500000. Ukichukua 15 tu wa kusimamia ml 1 na utabakiza 500000 ambayo mtachanga na wafanga biashara wenzio nauli ya gari coz huoakii peke ako.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Hao ng'ombe unaowaona hapo pugu wakubwa na wanono ni process mkuu...... Hununuliwa wakiwa wadogo au wamekonda na kulishwa vizuri kwa kipindi fulani kabla ya kuuzwa tena au kusafirishwa kuja hapo pugu........ Kwa kawaida kununua ng'ombe aliyekamilika ni ghali na ngumu kuwapata kwani wafugaji huuza ng'ombe dhaifu na wadogo na mara chache wazuri kwa dharura!!! Biashara hii ni nzuri kama utakuwa na reliable source ya kuwapata kwa bei poa..... Obheja nkwela!!!
 
Tena siku hizi wala hakuna kuhangaika kupeleka huko
Ukipata wanunuzi wa Dar wanakuja hapo hapo na kubeba mzigo na faida yako unaiona tayari
Unaingia tena kutafuta
Mbona inalipa vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…