Nina mtoto naye wa miezi 9 na ninampenda, ila anamwanamke mwingine na mtoto wa miezi 11, nifanyaje?

Nina mtoto naye wa miezi 9 na ninampenda, ila anamwanamke mwingine na mtoto wa miezi 11, nifanyaje?

Bi dentamol

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
1,018
Reaction score
2,130
Ninamtoto nae wa miez 9, tuko nae mikoa tofauti nampenda sana. Huyu kaka ni muhuni sana anamwanamke tena kazaa nae anamtoto wa miez 11 yeye wanafanya nae kazi sehemu moja. Huyu jamaa nampenda sana japo yeye haonyeshi interest ya kuishi na mimi najikuta na wakati mgumu kwani pamoja na tabia yake bado nampenda sana .

Anavyo onekana anampenda yule mwanamke japo hawaishi pamoja, moyo wangu unakua mgumu kumuacha sijui nifanyaje kwani najua kabisa hanipendi yupo kwa ajil ya mwanae tu isitoshe naona na nae mara 1 kwa miezi hata 5 but sijui kwanini nampenda to death, niendelee tu kubanana hapa hapa labda anaweza akanioa au nifanyeje maana naeza panga kuacha kabisa baada ya siku 2 nashindwa nakuta namtafuta tena.

Please naombeni mawazo yenu

NB: Huyu ni ndugu yangu wa damu kabisa binafsi nimeshindwa jinsi ya kumshauri hebu nisaidieni nimwambieje huyu mtu?
 
Ha ha ha jibu mbona liko wazi hapo lady in action.. She should follow her head not heart.. Hajasikia yale maneno "moyo utakupeleka kaburini".. Inajulikana ni shida sana moyo unapopenda usipopendwa lakini ifike wakati akili ikuzindue mapenzi ya isidingo kwenye real life ni kusadikika..

Anachohitaji kufanya ni kuhamishia mapenzi kwa mtoto wake huyo.. Bahati nzuri penzi lake kwa jamaa limempa zawadi ya mtoto.. Maisha ni zaidi ya mapenzi, anachotakiwa ajitahidi kupambana na kuudhibiti moyo wake.. Mwisho wa siku atakuwa huru kabisa..
 
Mwambie aendelee kujing'anganiza tu hapo hapo akija kushtuka alfajiri. ...maana si anajifanya yeye ni bingwa wa kupenda???
 
Subiri akukanyagishe miwaya mpendwa,hapo ndo utapojua maharage mboga au futari...
 
Ukitaka kuishi kwa furaha kwenye mahusiano au ndoa penda unapopendwa, mahali ambapo hupendwi achana nako. Lea mtoto wako fanya mambo yako acha kumshobokea mtu asiye kupenda.
 
Ni ngumu sana kuamini/kukubali kuwa unaempenda hakupendi/haoneshi interest na wewe. Ni wanawake wachache sana wenye upendo wa hivyo siku hizi.

Huyo mdada akubali matokeo na ku-move on painfully. Baada ya muda ata-cool off na kusahau maumivu yote. The world is never fair sometimes.
 
Unaweza kumpeleka mbuzi malishoni lakini kula majani ni khiyari yake,sasa mpaka yeye mwenyewe aseme imetosha hakuna atakaeweza kumtoa hapo,asikushughulishe sana yeye mwenyewe anajua nini anapenda nini anapewa na nini khasa kilicho mgandisha kwa huyu bwana,sasa wewe hata ukimshauri ni sawa na kumpigia mbuzi gita wala hafahamu unasema nini...
 
Una shida kubwaa aiseee
 

Attachments

  • Share2015-03-17-889b2d151535d4b452ae3be092f5f68fd0cec05d26f3f13925a7bcb7ef520e58-Picture_jpg.jpg
    Share2015-03-17-889b2d151535d4b452ae3be092f5f68fd0cec05d26f3f13925a7bcb7ef520e58-Picture_jpg.jpg
    11.9 KB · Views: 224
Aiseee!sasa wajua hupendwi wangangania nn mwenzangu wataka akuue kwa maradhi ndo roho itakutulia?
 
Back
Top Bottom