255Capacity
Member
- Jun 6, 2021
- 25
- 19
Hyo koz uliyosom mbna haiko na competition sana, tatiz ni nn mkuu
Wizara ya afya wametangaza ajira. Omba data manager. Kazi zipo nyingi Sana serekalini na NGOs wanahitajika Sana watu wa data ,hesabu.Habarini wanajamvi wenzangu,
Vijana wenzangu, wadogo Zangu na wakubwa Zangu, ndugu jamaa na marafiki nimekuja jukwaani humu kuomba msaada kwa yeyote ambaye anaweza kunisaidia kupata kazi/Connection yoyote halali popote ndani ya Tanzania hii ninaomba anisaidie baada ya kuumaliza shahada yangu ya kwanza nilijiunga na Jeshi la kujenga taifa (JKT) nimefanya mafunzo na majukumu mbalimbali ndani ya chombo hicho kwa miaka mi3 kuanzia Nov 2017- Dec 2020 bahati mbaya sikubahatika kupata ajira katika vyombo vya ulinzi na usalama paka mkataba wangu ulipomalizika kwa Sasa nipo Mkoani Arusha.
Umri wangu: 29yrs
Elimu: Shahada katika Uchumi na Takwimu.
Niko teyari kufanya shughuli Yeyote halali mahali popote ndani na Tanzania bila kujali elimu yangu, mazingira wala changamoto mpya.
Sifa
Mwepesi kujifunza vitu vipya, mchapa kazi, Mwaminifu, mcha Mungu, mstahimilivu,mtu wa kufocus kakika kupata matoke chanya katika utendaji lakini pia msiri.
Kwa Yeyote mwenye kuweza kunisaidia au kunishika mkono au hata kunionyesha njia ya kupita tafadhali ninaomba anisaidie na Mimi naahidi sitamwangusha ukinipm nikipata ujumbe wako nitakujibu kwa wakati kwa Jambo lolote kuhusina na uzi huu ikiwemo hata ushauri karibuni sana.
Natanguliza shukrani Zangu za dhati kwenu nyote.
Hyo koz uliyosom mbna haiko na competition sana, tatiz ni nn mkuu
Serikali inabana matumizi, pesa hakuna.Nimegundua jambo, kuna watakwimu wengi sana mtaani.Kuanzia ngazi ya cheti mpaka ngazi ya uzamili.
Suluhisho la muda, uandikwe muswada kwenda wizara ya fedha, idara ya takwimu taifa, na wizara ya kazi, ajira na maendeleo kwa vijana wapewe kipaumbele katika nafasi za zoezi la sensa mwaka 2022,
Kuliko kuwatumia Waalimu wa shule za msingi na sekondari ambao tayari wanaajira mkononi.
Hayo ni Maoni yangu, unaweza kuwa na maoni yako pia.
Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app