Kama mbeya uende na kurudi ila ulale standNdugu zangu,
Nataka kwenda sehemu yoyote Tanzania nikapumzike kwa wiki moja. Bajeti yangu ni kama Shilingi 200,000/= hivi. Je inawezekana kwa bajeti hiyo?
Matarajio yangu ni haya.
1. Sehemu hiyo iwe na mandhari nzuri za asili. Nataka nitembee, niexperience maisha ya kawaida ya watu, nipoze akili kidogo.
2. Vyakula viwe vizuri ila visivyo na gharama sana. Nyama au samaki pamoja na matunda viwepo kwa wingi.
3. Malazi yawe safi na salama ila ya gharama za kawaida. Ningependa kukaa lodge safi.
Vipaumbele vyangu ni sehemu moja kati ya Iringa, Mbeya, Bukoba na Mwanza ingawa niko tayari kupafikiria na pengine.
Labda tembelea ofisi za CCM lumumba ukashangae shangae mafisadi yaliyo vaa nguo za kijaniNdugu zangu,
Nataka kwenda sehemu yoyote Tanzania nikapumzike kwa wiki moja. Bajeti yangu ni kama Shilingi 200,000/= hivi. Je inawezekana kwa bajeti hiyo?
Matarajio yangu ni haya.
1. Sehemu hiyo iwe na mandhari nzuri za asili. Nataka nitembee, niexperience maisha ya kawaida ya watu, nipoze akili kidogo.
2. Vyakula viwe vizuri ila visivyo na gharama sana. Nyama au samaki pamoja na matunda viwepo kwa wingi.
3. Malazi yawe safi na salama ila ya gharama za kawaida. Ningependa kukaa lodge safi.
Vipaumbele vyangu ni sehemu moja kati ya Iringa, Mbeya, Bukoba na Mwanza ingawa niko tayari kupafikiria na pengine.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Sikia mchizi wangu, njoo huku porini kwangu, tutalala kwenue kibanda changubcha nyasi, nina kitanda cha kamba cha ziada hicho utatumia (sijakitumia muda mreeefu kama kitazingua, nitalala kwenye mkeka we utalala kwenye tendegu langu) hiyo laki 2 tununua viroba vya unga, mchele na mafuta, maharagwe nakadhalika, hapa utakaa zaidi ya muda wako, mimi ndio nitakuwa tua gaida wako, nakuzungusha kijijini kote na mademu wa huku wakiona mgeni wa mjini hawamnyimi.
Karibu sana mzee.
Kwakweli, hapana sidhani kama kuna la kuenjoy. Nenda zenj MkuuNikisema niongeze, panafaa lakini kwa mapumziko na kuenjoy?
Umetisha mkuu. Kitulo pamenivutia sana. Ila naona kama patapendeza zaidi nikija na kampani fulani hivi.Duh hii pesa ndogo Sana sana kwa hio miji, Njoo hapa Njombe utalala Guest za kawaida, then utaenda Kitulo-Makete kwa nauli ya 15,000, kiingilio 30,000, accomodation utarudi mtaaani utalala kwa 20,000. Kuna baridi sana hivyo Maji ya buku yanakutosha sana kwa siku.
Breakdown hii hapa.
1. Nauli.
1.1. Dar-Njombe kwenda na kurudi plus bodaboda hivi weka 90,000
1.2. Njombe-Makete kwenda na kurudi weka 30,000 na bodaboda humo humo
1.3. Makete-Kitulo kwenda na kurudi 12,000
2. Accomodation.
2.1. Malazi one night in Njombe 20,000
2.2. Malazi two nights in Makete 40,000
2.3. Malazi one night in Njombe 20,000 (wakati wa kurudi Dar)
3. Meals.
3.1. meals in Njombe Wakati wa kwenda 20,000
3.2. Meals in Makete weka 20,000
4. Entrance fee.
Kitulo Entrance fee weka 30,000
5. Incidentals.
Weka kama 20,000 minimum
Jumla
Approximately uwe na 300,000 -350,000 utakua umefika Kitulo kwenye World Garden of Flowers
The same budget unaweza kwenda Lushoto -Tanga Kuna falls, Kuna Irente View, Kuna misitu ya asili AU uende AMANI -MUHEZA-TANGA kwenye misitu ya asili na vipepeo ambao hawapatikani popote pale pengine AU uende Tanga Amboni, au uende hapo Morogoro Mikumi National Park kwenda Na Kurudi.