Nina Shilingi 200,000; wapi naweza kwenda kutalii kwa bajeti hiyo?

Bukoba kwenda na kurudi nauli tu ni 160,000/= ukiweka na chakula cha njiani basi hiyo 200k ni nauli ya kwenda na kurudi labda upande bajaji. Assumption ni kuwa uko Dar.
 
Mkuu kwa bukoba nakushauri usiende bukoba mjini nenda mtukula boda la uganda utainjoy sana...lkn km unataka kushangaa mazingira na kula samaki kwa wingi nenda mwanza

Ila kwa hyo bajeti kwa wiki 1 ni ndoga sana
Kwa lodge ya 15000 kwa cku 7 ni 105000 hapo bado nauli chakula vinywaji hapo nimeashum ww co mtu wa totoz..!!!
 
nenda mbagala
 
Nenda Kisarawe anzia Pugu hills hadi Minaki na huko Pond.Kuna camping sites utalala hemani.
 
Nenda Tabata ukafanye 'utalii wa ndani'.
Anzia kiwanja cha familia kinaitwa 'GBF' upate supu ya motomoto, pata moja baridi mahali panaitwa 'The Great' halafu shuka kidogo uende Kitambaa Cheupe (Kwa Jesca) ukajionee 'wanyama mbugani' na Buzuku la kufa mtu, halafu jisogeze ukajimalize mwenyewe kwenye kiwanja matata sana kinachotikisa Tabata nzima kwa sasa kinaitwa "Small Planet" kakeshe pale hadi majogoo, na kisha kamalizie usingizi wako Tabata Center Point. Ukiamka asubuhi siku ya pili ukiamka, anzia kiwanja wa watu wazima au kwa wazee wa Tabata panaitwa Mperani aka Kwa Mrosso ujipatie kichwa cha mbuzi, halafu nenda Bwawani kwenye miti, kisha pitia Mr. Wine kidogo na uende ukalale Tabata Hotel

200,000/- itakuwa imeisha
 
Nenda Kisarawe anzia Pugu hills hadi Minaki na huko Pond.Kuna camping sites utalala hemani.
Nimeipenda hii. Wanachaji kiasi gani kulala hemani?

Matangazo ninayoyaonaga ya Kisarawe Kazimzumbi huwa gharama ziko juu na tena huwa hawalali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…