Nina Shilingi 200,000; wapi naweza kwenda kutalii kwa bajeti hiyo?

Hapa Arusha Kuna watoto wa shule ya msingi wanachangishwaga 50K wanapakiwa kwenye coaster wanapelekwa manyara kuosha macho na kurudi jion nenda kajiandikishe kwa watoto wa darasa la pili uende nao chenji yako ununue popcorn
 
Anza kufikiria Sehemu ya kulala na umesisitiza iwe nzuri, means haiwezi kuwa chini ya 50k na unatarajia ukae week 2...kwa siku utakula Shingapi? Nenda kisarawe Bro
 
Nenda Bagamoyo, kila ulichosema kipo, mji mdogo, wakazi wenye maisha ya kawaida, mandhari nzuri, historia, ufukwe, chakula bei rahisi na hoteli tulivu za gharama za kawaida, halafu ni nje tu ya jiji

Nakubaliana na wewe niliwahi pata huduma ya kutembezwa kwenye historical sites pale Bahamoyo
Kwa 20,000 tu na kuna hotel nzuri ambazo unalala kwa 20,000-30,000 tu

Kama yupo Dar basi aende Bagamoyo, kama yuko Mikoa ya nyanda za juu kusini aende kitulo National park.
 
Laki 2 ni ndogo sana mkuu, ILa kwa Zenj ikiwa utatufa zile loge 20 kwa siku na ukawa unakula kwa mama ntilie, unaweza kupata chance ya kwenda kupiga makachu beach.
Makachu ndiyo nini mkuu?
 
Kwa pesa hiyo wewe nenda buza tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…