Nina shilingi mil 8 nishaurini biashara ya kufanya

Nina shilingi mil 8 nishaurini biashara ya kufanya

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,917
Reaction score
11,801
Wakuu kulingana na serikali ya Tanzania kutokuwajali wafanyakazi wake nimeamua niache kazi nifanye biashara, sasa nina kiasi tajwa hapo juu nianze na biashara gani nzuri ushauri wako plzz.
 
Wakuu kulingana na serikali ya Tanzania kutokuwajali wafanyakazi wake nimeamua niache kazi nifanye biashara, sasa nina kiasi tajwa hapo juu nianze na biashara gani nzuri ushauri wako plzz.
Mkuu kabla ya kuacha kazi ulitakiwa kujua unataka kufanya nini au kuomba ushauri kabla ya kuacha kazi. Usipoangalia hela yote utaila kabla hata hujapata hilo wazo unless kama nimekuelewa vibaya!!
Nukta
 
Njoo malinyi ununue mpunga kwa 42000 kwa gunia bei ikipanda unauza gunia kwa 80000 mpaka 90000
 
Fanya biashara ya kunikopesha kwa riba ya 0.001% kwa mwezi , ntamaliza deni lako baada y amiaka 8.
 
Sijaacha kazi ila nafikria kufanya hivyo ili niweze kujiajiri, nipo kanda ya ziwa.
 
jiingize mazima kwenye kilimo na ufugaji, huku ukiangalia fursa zinazopatikana katika eneo lako la kijiografia!
 
kama upo town ufugaji wa kuku wa mayai unalipa sana tu....ukiwa na kuku wa mayai around 200 utatengeneza net profit not less than kilo saba mpaka saba na nusu kwa mwezi...
 
kama upo town ufugaji wa kuku wa mayai unalipa sana tu....ukiwa na kuku wa mayai around 200 utatengeneza net profit not less than kilo saba mpaka saba na nusu kwa mwezi...
You're not serious. Nipatie mchanganuo wa jinsi kuku 200 wanavyoweza kukupa faida hiyo (baada ya kutoa gharama za uendeshaji) nianze biashara hiyo mara moja.
 
Mkuu wewe ndo unatakiwa kutafuta wazo bora kabisa la biashara, wazo bora linatoka kwako mkuu, Ni wewe unaye jua mazingira ya hapo ulipo, ni wewe unaye jua jamii yako inapungukiwa na nini? au kwa miaka ijao itapungukiwa au itahitaji huduma fulani,

Wazo hutokana na Mazingira uliopo, na kinyume na hapo unatafuta shida,

Na unatakiw akujikitakutatua matatizo yanyo kumba jamii uliopo, mambo ya pesa huwa ni matokeo, na mara nyingi watu hukata tamaa ya biashara kwa sababu wao wliingia na lengo moja tu kutafuta faida, na faida inapo kuwa haijapatikana kwa muda mwafaka mtu huchanganyikiwa,

HIVYO ANGALIA MZINGIRA YA HUKO KANDA YA ZIWA AU AHALI UNAPO KAA NA UTAPATA WAZO BORA KABISA, NA LINATAKIWA KUWA WAZO ENEDELEVU SIO ZIMA MOTO

Wazo la Biashara halihitaji kupiga lamuli,
 
Hakika. Malinyi, mtimbira na Lupiro ni Kwa ukweli.

ukikosa hapo chomokea... Tanganyika masagati ( kwao Balali wa BOT), mpanga, mlimba, mgeta, chita n.k lazima mpunga ni mwingi sanaa
 
Back
Top Bottom