Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kitu kimoja nimeona Mbeya tofauti na mikoa mingine ni wingi wa Bajaji hizi na bodaboda. Ni nyingi hadi zinakera. Naambiwa kwamba wingi wake umeletwa na Tulia Foundation ya spika wa Bunge ambaye amekuwa akiwawezsha vijana hapa mkoani, yote haya yakiwa ni katika kuungwa mkono dhidi ya Sugu!
Sawa. ni jambo zuri Tulia alifanya. Lakini sasa ameleta kero nyingine, maana sasa hawa watu waliokuwa na lengo la kufanya biashara ya bajaji na bodoboda, wamejikuta wako kwenye ushindani mwingi wa kupata abiria na sasa bajaji na bodaboda havilipi tena. Hawa waendesha pikikipi wameanza kukwapua mifuko ya watu barabarani, na hasa handbag za kina mama! Siku tatu tu hapa tayari nimeona matukio matano ya ukwapuaji handbag za wanawake! Nadhani baada ya muda mfupi Mbeya itakuwa inaongoza kwa aina hii ya wizi.
Natoa tahadhari kwa wakazi wa Mbeya na mnaokuja kutembea kama mimi - chunga begi lako au handbag yako. La sivyo utakuta umeporwa, kutia ndani laptop bags. Usitembee barabarani kwa madoido ukiwa umening'iniza begi au handbag begani hapa, watakuliza!