Nina sumbuliwa na tumbo kwa mda mrefu sana

Nina sumbuliwa na tumbo kwa mda mrefu sana

Joined
Jan 8, 2014
Posts
93
Reaction score
32
Salaam.
Ndugu wana jf naomba msaada wenu tafadhali, kwa muda usiopungua miaka kama mitano nimekuwa nasumbuliwa na maumivu ya tumbo mara kwa mara. Nimejaribu kwenda hospital kadhaa lakini nimeambiwa hamna tatizo.

Moja ya dalili zisizo za kawaida nazo zipata ni kama vile,kutopata choo vizuri na mda mwingine huambatana na vitu vyeupe mfano kama mucus, tumbo kujaa gesi na kuuma na kujihisi kwenda msalani lakini unakuta choo hakitoki zaid ya gesi, pia tumbo huuma haswa wakati wa baridi.

NAOMBA MSAADA WENU WAKUU.
 
Hiyo inaweza kuwa ni IBS yaani Irritable Bowel Syndrome, hiyo kitu inasumbua sana, hospital inaonekana hawaiwezi sasa sijajua kama hawa wataalamu wa tiba ya asili kama wanaweza kuitibu kwanza hata chanzo chake hakijulikani na hakuna kipimo cha kuipima hiyo, yaani huwa inakuwa diagnosis kwa symptoms tu, ni type ya digestive disorders... labda mkuu MziziMkavu anaweza saidia zaidi, au hata Mimi49 anaweza pitia hapa kutoa ushauri zaidi

sana sana hospital utakuwa unapewa madawa ya kutibu dalili tu...
 
Last edited by a moderator:
Salaam.
Ndugu wana jf naomba msaada wenu tafadhali, kwa muda usiopungua miaka kama mitano nimekuwa nasumbuliwa na maumivu ya tumbo mara kwa mara. Nimejaribu kwenda hospital kadhaa lakini nimeambiwa hamna tatizo.

Moja ya dalili zisizo za kawaida nazo zipata ni kama vile,kutopata choo vizuri na mda mwingine huambatana na vitu vyeupe mfano kama mucus, tumbo kujaa gesi na kuuma na kujihisi kwenda msalani lakini unakuta choo hakitoki zaid ya gesi, pia tumbo huuma haswa wakati wa baridi.

NAOMBA MSAADA WENU WAKUU.
Tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation)...

UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu. Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?
Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa. Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

NINI HUSABABISHA TATIZO?
Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

NINI KIFANYIKE?
Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda msalani. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil’ muda mfupi kabla ya kwenda kulala. Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.
 
TIBA:


Kanuni ya kwanza


1.Chukua glasi moja ya maziwa freshi baridi uchanganye na vijiko viwili vikubwa vya asali na kijiko kimoja kidogo cha mafuta ya habitsoda. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Dawa hii hufanya choo kuwa laini na kupata haja kubwa kwa wepesi.


Kanuni ya pili:


2.Unga wa sanamaki kijiko kimoja kikubwa, Unga wa tangawizi kijiko kimoja kikubwa, Unga wa habasoda kijiko kimoja kikubwa, na Asali robo lita. Dawa hizi zote zichanganye pamoja kwa kukoroga kwa kijiko. Kula kijiko kimoja kutwa mara tatu.


Kanuni ya tatu:


3.Asali robo lita, na Unga wa Arki susi vijiko vinne vikubwa. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara mbili.


Kanuni ya nne:

4.Kunywa kwa wingi maji ya Uvuguvugu ya kutosha na pia ule kwa wingi matunda na mboga.


Kanuni ya tano:

5.Kula kila siku asubuhi tende saba kabla ya chakula cha asubuhi. Tende hufanya choo kuwa laini. INSHAALLAH UTAPONA.

CHAGUWA TIBA MOJAWAPO KWAKO WEWE ITAKUWA NI RAHISI KUIPATA TUMIA KWAMUDA WA SIKU 3 HUKUPONA

CHUKUWA MAELEZO YA TIBA INGINE HAPO FANYA HIVYO HIVYO MPAKA UTAKAPO PONA.
@ Shuaibu yahaya
 
Back
Top Bottom