Elimu hii inafahamika kama QT (Qualifying Test)
Vigezo
Mtu yeyote aliyehitimu darasa la saba au chini ya hapo, Mimi nilisoma sikuulizwa cheti cha darasa la saba pia nilisoma na ambao hawakuwa wamehitimu darasa la saba.
Utaratibu wa Masomo
Mwaka wa kwanza:'
Utajifunza masomo yote tisa ya kidato cha kwanza na pili kisha utafanya mtihani wa QT ili uweze kuendelea na mwaka unaofuata kusoma Masomo ya kidato cha tatu na nne.
Mtihani wa QT unafanyika siku moja, na ni mtihani unaojumuisha Masomo yote tisa kwenye karatasi moja ila mtahiniwa atachagua masomo matano tu kati ya tisa Ndiyo atakayojibu.
Mtihani unavyofanyika
Mtihani unamasomo tisa na unafanyika ndani ya masaa matatu, English, Kiswahili, Civics, History, Geography, Mathematics, Chemistry, Biology, Physics
Kwenye mtihani huo Kiswahili, civics na English ni lazima kujibu. Kisha utachagua masomo mengine mawili yanayoendana ili kukamilisha masomo matano
Iko hivi so utachagua mwenyewe ufanye kundi lipi
-English, kiswahili,civics Geography na History
-English, Kiswahili, civics Chemistry na Biology
-English, kiswahili, civics Mathematics na Physics
Unahitaji maksi kama 50-60 kwa masomo matano uliyofanyia mtihani kufaulu.
Mwaka wa pili
Ukishafaulu mtihani wa QT utaendelea na masomo ya kidato cha tatu na nne kisha utafanya mtihani wa kidato cha nne.
Gharama
Niliposoma mimi walitoza 500,000 kwa mwaka na ada ya mtihani isiyozidi 50,000. Walikuwa na madarasa, walimu wa masomo yote, na nyenzo za kujifunza kwa vitendo kwa masomo ya sayansi.
NB; Mwaka wa kwanza ni rahisi sana, usipofaulu ni uzembe wako, ila mziki upo mwaka wa pili unaposoma Masomo ya kidato cha tatu na nne.