Subiri ipo siku, mimi nilikuwa hivyo hivyo na huruma ....kuna siku jamaa mmoja alinikuta nimekaa sehemu akaja anatia huruma sana ana nihadithia ana siku ya 3 hajala chochote , anasema alikuwa anaishi na mama yke wa kambo huko Mwanza baba yke alipo alifariki sasa baba yke alipo fariki tu mama wa Kambo akamfukuza , kwakweli alinihadithia vitu vingi ambavyo vinatia imani na huruma na huyu kijana alikuwa na umri wa miaka kama 17 hivi , kwanza nilimnunulia chakula, alishukuru sana tena alikuwa anataka kupiga magoti nikamkatza , yule dogo kutokana na muonekano wake na jinsi anavyotia huruma nikaona nimsaidie...
Nikaamua niishi nae geto....tulikaa sana yapata mwaka 1 mpk nikaanzisha biashara akawa ana simamia vzr kwa uaminifu tu na mimi nikazid kumwamini .....sasa kutokana na mishe zangu zingine ilibid kijana nimtume kwenda kufungasha mzigo ..mara ya kwanza, pili na ya tatu alienda akarud vzr tu biashara ikakua, nikazid kumwamini ilibid tuongeze mzigo uwe mkubwa kwani wateja wamekuwa wengi .....ilibid nimtume akachukue mzigo tena kibunda cha kutosha ...nilimpatia ....yaani tangu siku hiyo tarehe 17.06.2014 mpk leo huyo kijana hajawah kurud na sijui alienda wapi...nimemtafuta mpk nimekata tamaa , isitoshe aliondoka mpk na vitu vingine pale geto ...kwn siku hiyo anaondoka mimi nilikuwa job. Sasa watu hawaaminiki jombaa