Nina tatizo gani mimi? Napenda sana kuwa peke yangu

Mwalupale

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2012
Posts
1,049
Reaction score
674
Habari zenu wanabodi,

Kwa miaka ya hivi karibuni nimekuwa napenda sana kuwa peke yangu. Iwe kazini, shuleni (nasoma chuo), kwenye sherehe, nyumbani au sehem yoyote ile. Hata nikiwa na mgeni home kwangu natamani aondoke.

Haijalishi nigeni wa kiume au wa kike. All i need is to be alone and make my own reflection of this life. Nimekuwa out of touch kwenye communication na mpenzi wangu na amekuwa mtu wa kulalamika tu. Ndugu zangu na wanafamilia wangu ndio kabisaaa mpka wanitafute wenyewe.

Nimekuwa mvivu wa kuongea kwenye simu. Mtu akinipigia nataka aongee shida yake chap chap na akate simu.

Je, hili ni tatizo gani wakuu? Msaada please.
 
Ukiwa mwenyewe unapenda kufanya nini? Maana pia mimi most of the time niko alone na nina enjoy, nitaangalia movies, nitasoma, nita swim na ku take a long walk on the beach on my own! Na nina furahia sana maisha, naamini usemi wa raha jipe mwenyewe. Kama una enjoy the company of me, myself and I that is totally gr8 my friend! Ubarikiwe sana
 
Ni kipindi katika makuzi kitapita, ila uamuzi utakaochukua sasa ndio utakuwa haiba yako
Mkuu mshana jr hebu tupe somo juu la hili jambo japo kidogo, hata mimi nimo kwenye hili kundi la kutaka kuwa mpweke wakati wote. Lakini mimi nipo tofauti kidogo na huyu mleta mada sababu zangu za kuwa nataka kuwa peke yangu ni hizi:-
1 Rafiki zangu niliokulia nao wengi wapo mbali na mimi.
2 Rafiki hawa niliojuana nao ukubwani wengi wadaku(Shilawadu team)
3 Nipo sana kwenye mtandao lakini nafatilia sana mambo ya kutengeneza hela hasa kununua hisa na kuuza.
4 Gym ndio sehemu yangu kuu lakini sipendi kuongea na mtu kutokana nimekwenda kufanya mazoezi.
5 Napenda kwenda club(kumbi za muziki) lakini nimeamua kuacha pombe, na nikiona kimada huingia tamaa ya kuzini kwahio nimeamua kuacha kwenda.
 
Hapo kuna mengi umechukua mengi mazuri, umejitambua na kuamua kujireshape for the better of yourself, vizuri sana
Jitahidi uwe na marafiki wachache positive ones
Kuhusu libido ni kwa vile umri unaruhudu unakula vizuri na huna stress nyingi hivyo it's natural
 
Nakushauri acha hiyo tabia ......na bila shaka una vidonda vya tumbo au chembe ya moyo....nimesema hivo kwasababu.....
Vidonda vya tumbo na hiyo chembe ya moyo ninayo. Nisaidie namna ya kuacha mkuu
 
Hizo ni dalili za kwamba wewe ni genious!
Kuna uwezekano mkubwa pia kuwa uko prone kupata ugonjwa wa Depression...
Mimi ni genius kiasi. Nimefaulu sana masomo ya sekondari, nina first class degree kwenye bachelor yangu ya kwanza, kwasasa nasoma masters na semesters zangu zinang'aa vizuri
 
Tuna hali inayotaka kufanana, sidhani kama ni tatizo hili. Mimi sikumbuki ilianza lini ila tu nilikua nikajikuta hivyo. Sina wasiwasi na hii tabia na sifikirii kuitafutia tiba. Otherwise labda utuambie una dalili za depression mkuu.
 
pole mkuu unaugonjwa wa upemwi
ukosefu wa pesa mwilini ndio mana huna amani unajitenga na watu.
hebu tuambie ukiwa peke yako unapenda kufanya nini?
Nikiwa pekeangu napenda kujisomea vitabu mbalimbali, kuperuzi mtandaoni, kuandika stories na kulala.
 
Asante mkuu. Lakini nimekuwa nahisi kama ni tatizo. Najiuliza Hii hali imetoka wapi wakati zamani sikuwa hivi. Kama wewe unaenjoy basi hongera sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…