Nina Tsh. milioni 200, niweke benki gani yenye 'Fixed Interest' nzuri?

Intrest rates za bank ya Nmb zikoje? Mkuu na mimi nina shida kama ya kwenu,nilienda crdb wao wakaniambia riba yao ni asilimia 5 tu mpaka mwili ukachoka
 
Intrest rates za bank ya Nmb zikoje? Mkuu na mimi nina shida kama ya kwenu,nilienda crdb wao wakaniambia riba yao ni asilimia 5 tu mpaka mwili ukachoka
Pia wana bonus account ambayo hukatwi na interest ni 3.5 mpaka 5.5 kutegemea hela unayoweka. Unapata interest quarterly na sharti ni utoe hela mara moja tu katika miezi mitatu. Tofauti na fixed hii unaweza toa hela muda wowote japo ni lazima uende dirishani
 
Ushauri wangu nenda makao makuu ya benki hizi kubwa then negotiate nao kuhusu interest rate. Usiende kwenye matawi nenda kwa watunga sera wanaweza kukupa special rates. Hiyo hela ni nyingi unakuwa na power ya ku negotiate

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Intrest rates za bank ya Nmb zikoje? Mkuu na mimi nina shida kama ya kwenu,nilienda crdb wao wakaniambia riba yao ni asilimia 5 tu mpaka mwili ukachoka
Nenda BankABC kama unaamini kuwa the higher the risk the higher the return mim nimesaini this morning their rate is above 10% and is negotiable.
 
Mkuu hajasema hana uwezo wa kuitunza ila anatafuta mahali ambapo anaweza kuongeza hicho kiasi kuliko kukaa nayo nyumbani wakati anafikiria afanye nini?
Pia angesema ameipataje hiyo 200m. Zaidi ya hapo ni swaga tu. Huwezi kumiliki 200m pasipo kujua kuziendeleza huenda kama ni za kiinua mgongo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani badala ya kujibu swali wanapandikiza mawazo yao na hivyo kupotosha wazo la mtoa mada, FIXED DEPOSIT.
 
Watu wataogopa kuona kuwa wewe
Ni member wala sio jf expert wanataka platinum members
 
Bank gani chief
Ilikua barclays, for now sijui kutokana na mabadiliko ya kibenki. By the way, 15m unaweza invest katika business unaweza tengeneza that amount monthly as a profit not sales, monthly.
 

Duh ! Kaka miaka mitano iliyopita ungeanza biashara na ukaisimamia vyema ungekuwa umepata mara 100 ya hiyo 8 M.

kweli sijawahi kuthamini biashara ya kununua viwanja now na kuuza baadae kwa lengo la kupata faida. Kama unafanya hivyo kwa lengo la urith sawa.

mfano unasikia magomeni kiwanja ni Mil 150, but wengi wanaopata hizo hela sio wamiliki, ni wajukuu.

Wamiliki walishakufa zamani . It is not not good business to start.


Mk54
 
Najua lengo lako la kuitia yote hyo mbal na faida ila n sehemu salama 100%... Ila mkuu ikikupendeza unaweza toa fungu hapo ukanunua hisa za crdb hutokuja jutiaaa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama lengo ni kuhifadhi basi weka Bank yoyote ila kama unahitaji kupata faida sikushahuri kuweka Fixed, weka NMB Bonus Account. Lakini kama unategemea kuanzisha mradi basi weka akaunti yoyote utakayoweza kutoa pindi utakapohitaji fedha zako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…