Nina Tshs. 45 milioni, Nifanye biashara gani?

sikuwa na mpango wa kuingia humu leo lakini nimevutiwa na kushawishiwa na juhudi zako na wife wako..kwanza labda nikuulize unaishi wapi ili angalau hata mtu akitaka kukushauri kuhusu hiyo miradi mingine labda direction inaweza kusaidia..

pili kwa maelezo yako na msisitizo ulioweka kuwa lazima ifanyike maeneo ya nyumbani, mi nakushauri uendelee na hiyo hiyo baishara ya kuku, wala usiogope wala usitishike na hizo changamoto..

ila nikuullize jambo moja umeshafanya physical survey/search ya soko wewe mwenyewe? achana na media tembelea soko hilo la kuku/mayai na uone mwenyewe, au zungumza na wafugaji wakupe data za ukweli na pia unapokuwa sokoni utajifunza mbinu za kukabiliana na changamoto nyingi, mfano ikibidi unaweza kupunguza bei kidogo ili uatract wateja zaidi ilimradi tu kuhakikisha hakuna hasara..

hii biashara ya kuku ni nzuri we endelea na plan yako, na hongera kwa mafanikio
 
ni nzuri ukitafuta hizi biashara za kuwa wakala au msambazaji kwa kampuni mbalimbali za hapa nchini na nje ya nchi,na unaweza kupata taarifa hzo za kampuni zinazotafuta agent/distributors hapa www.mpakasi.com kuna fursa mbalimbali za kibiashara
 
Jikite katika kilimo,ufugaji..viwe vya kitaalamu zaidi,utaona matokeo makubwa na ya faida kubwa.

Ila usimamizi muhimu juu ya hayo nakufuata ushauri wa wataalamu.
Au Invest katikia Biashara za Nafaka fulani fulani.

Note.
 
Nawashukuru sana wadau mliokwisha changia mada hii na wale watakaoendelea kuchangia. Mwisho wa siku nitachuja mawazo yenu mliyoyatoa kwa nia njema na kwa umakini na hatimae kuibuka na maamuzi muafaka. Kwa pamoja tutajenga.
 
wewe sio mwenzetu kabisa,yani mshahara wako umaweza uka-save? Kabla sijachangia ebu tuambie kwa mwezi unapokea sh ngapi kama salary?
 
Kwa kuwa unataka mradi ufanyikie nyumbani kwako basi fuga nguruwe kama imani inaruhusu.
 
wewe sio mwenzetu kabisa,yani mshahara wako umaweza uka-save? Kabla sijachangia ebu tuambie kwa mwezi unapokea sh ngapi kama salary?

Ndugu yangu kuhusu kuweka hadharani kiasi cha mshahara wangu sidhani kama kutakusaidia chochote. Kwa hiyo sitakutajia. Naomba ushauri wako u base zaidi kwenye facts nilizokwisha ziweka hapa kama walivyofanya wana JF wengine waliokutangulia kuchangia mada hii. Nakutakia wikiendi njema.
 
Nyaka-One nimerudi tena kutoa ushauri mwingine mdogo na muhimu

Kwakuwa unahitaji project ambayo ni home based na Kwakuwa nyumbani pa kuishi hapapaswi kuwa na commercial scenes or environment hivyo basi unahitaji biashara ambayo the eyes of the regulators are very far or a business that is not easily regulated .... you can imagine the TRA on your foot steps

bado nasisitiza poultry venture itakuwa profitable and yes very lucrative .... hutapata adha ya kusumbuliwa na hawa watu Wa TRA, municipal licenses, TFDA and other regulators

apart from all your family will be guaranteed at least food supply for most of the daily life from the produce of poultry venture

I am in with experience and I started small but now its far from being a home based venture

all the best
 
Last edited by a moderator:
Bluetooth,
Ushauri wako kwenye mada hii hautapotea bure. Nakushukuru.
 
nilikuwekea wazo juu ya ufugaji wa kienyeji ila ile post siioni..
fuga kuku wa kienyeji pure Kisha nunua incubator utotoleshe kuku wakifika miezi 4-5 unachinja na kuuza katika hotels pia unafungua points ambazo utakua unauzia..kadri mzunguko utakavyokuwa mkubwa utaweza pia kuanza kusupply vifaranga wa kienyeji.
pia waweza kufuga bata nao wanafaida.
 
Jenga nyumba za kupanga au kuuza... there is no risk of losing all your money.
 

Thanks mkuu. Kutokana na mawazo ya wengi hapa naona wana support wazo la ufugaji nililokuwa nalo awali. Naona kuna haja ya kufanya thorough market survey kuhusu hili.
 
Mkuu kuna rafiki yangu anafanya hiyo biashara najaribu kuwasiliana nae ntakurudia hapahapa.Shukran
 

Mkuu chukua 15m jenga mabwawa matano ya samaki aina ya perege/sato. Baada ya miez 4 unaanza kula faida kiulaini. Hii biashara haina competitors wengi. Kwa ushauri mwingine wa kibiashara unipe laki 7 kama consultation fee. Kila la heri.
 
Fungua Guest house, wabongo penda sana mchepuko
 
kuna bank unaweka hela kwenye fixed deposit account na kisha unachukua 90% ya hiyo hela kuendelea na uwekezaji. kama utaweka mil 100 utapata mil 12 kwa mwaka. na mil 90 unaichukua kama mkopo unafanya biashara nyingine. PM Mimi.
Huo mkopo si utakuwa na interest na inaweza kuwa zaidi ya mil 12 kwa mwaka?
 
Watanzania hua hatunaga idea mpya ni zile zile kila siku fuga kuku,duka la hardware...kuna uzi ulikuwepo humu unazungumzia kununua treasury bills, bonds, kama vipi jaribu hayo mambo huo uzi wafuga kuku wote waliukimbia sio kwamba nabeza kufuga kuku lakini ni muda sasa biashara zibadilike sasa sio zile zile za photocopy..Over...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…